Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
MFUNGAJI bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simon Happygod Msuva amesema kwamba anaomba Mungu amsaidie aiwezeshe timu yake kutetea ubingwa na yeye kuwa tena kinara wa kufumania nyavu msimu huu.
“Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kufunga bao la kwanza la timu yangu msimu huu, tumeanza vizuri Ligi Kuu kwa ushindi na tunaomba Mungu atusaidie tuendelee hivi hivi hadi tutetee ubingwa wetu,”amesema Msuva akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE leo Dar es Salaam.
Alipoulizwa kuhusu kiu ya ufungaji bora, mchezaji huyo bora pia wa Ligi Kuu msimu uliopita, amesema kwamba atafurahia akipata mafanikio hayo na msimu huu.
“Nia ndiyo hiyo, ili tunamuomba Mungu kwa sababu yeye ndiye kila kitu. Kikubwa ninachofurahia ni mafanikio ya timu yangu,”amesema.
Yanga SC wameanza vizuri msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mabao ya Msuva na Donald Ngoma.
Matokeo hayo yanaipeleka Yanga SC kileleni mwa LIgi Kuu baada ya mechi nane za mzunguko wa kwanza, ikiongoza kwa wastani wa mabao.
Msuva ndiye aliyefunga bao la kwanza la Yanga SC msimu huu, dakika ya saba akimalizia pasi ya Amisi Tambwe kutokana na juhudi zake mwenyewe, baada kupokea pasi ya Haruna Niyonzima nje ya boksi na kuingia nayo ndani kabla ya kumpasia Tambwe aliyemrudishia mfungaji haraka kwa mbele kidogo.
Ngoma alifungia bao la pili dakika ya 42 na ushei akimalzia mpira uliodondoka baada ya kugongwa kwa kichwa na beki wa Coastal, Tumba Lui Swedi aliyeruka na Mrundi Amisi Tambwe kugombea krosi ya Simon Msuva.

Simon Msuva ameanza vyema msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara |

0 comments:
Post a Comment