MSHAMBULIAJI Basem Morsi (pichani) amefunga mabao matatu peke yake, Misri ikiichapa 5-1 Chad katika mchezo wa Kundi G kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika jioni ya leo Uwanja wa Omnisports Idriss Mahamat mjini Ouya.
Ushindi huo unaipandisha Misri kileleni mwa Kundi G baada ya kufikisha pointi sita kufuatia awali kuifunga Tanzania 3-0 Juni mwaka huu mjini Alexandria.
Nigeria ambao jana wametoa sare ya bila kufungana na Tanzania mjini Dar es Salaam sasa wanashika nafasi ya pili.
Tanzania wanashika nbafasi ya tatu, wakati Chad iliyofungwa 2-0 na Nigeria Juni inashika mkia.
Morsi alifunga mabao yake dakika ya pili, 25 na 62, mabao mengine yakufungwa na Mohamed Salah dakika ya 40 na 56 wakati bao pekee la Chad lilifungwa na Nadjim Haroum dakika ya 38.

0 comments:
Post a Comment