MECHI ZIJAZO LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
Jumamosi, Sept 19, 2015
Stand United Vs African Sports
Mgambo Shooting Vs Majimaji Fc
Prisons Vs Mbeya City
Yanga SC Vs JKT Ruvu
Jumapili Sept 20, 2015
Mwadui FC Vs Azam FC
Mtibwa Sugar Vs Ndanda FC
Simba SC Vs Kagera Sugar
Coastal Union Vs Toto Africans
Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
KOCHA wa JKT Ruvu, Freddy Felix Minziro amesema ana hasira za kupoteza mechi mbili za mwanzo za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Nyada za Juu Kusini, hivyo kesho atapambana ashinde mechi ya kwanza.
Baada ya kufungwa 1-0 na Majimaji mjini Songea na 3-0 na Mbeya City mjini Mbeya, JKT Ruvu kesho watacheza mechi ya tatu watakapomenyana na mabingwa watetezi, Yanga SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Na kuelekea mchezo huo, Minziro amesema; “Sisi tayari tumepoteza mechi mbili, japokuwa za ugenini, lakini tumepoteza. Sasa tunahitaji kushinda ili tukae sawa,”amesema.
Kuhusu Yanga SC, Minziro amesema; “Yanga SC ni timu nzuri, lakini ya kawaida tu kama timu nyingine na sisi tutaingia uwanjani kupambana nao bila woga, tunataka pointi tatu,”amesema.
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaendelea wikiendi hii kwa michezo nane kuchezwa Jumamosi na Jumapili katika viwanja nane tofauti nchini ikiwa ni mzunguko wa tatu tangu kuanza kwa ligi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mbali na Yanga na JKT Ruvu, mechi nyingine za Jumamosi ni kati ya Stand United na African Sports Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Mbeya City na Prisons Uwanja wa Sokoine, Mbeya, Mgambo Shooting na Majimaji FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Jumapili Simba SC watawakaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Mwadui FC watakuwa wenyeji wa Azam FC Uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga, Mtibwa Sugar watawakaribisha Ndanda FC ya Mtwara Uwanja wa Manungu, Turiani mjini Morogoro na Coastal Union watakuwa wenyeji wa Toto Africans Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Jumamosi, Sept 19, 2015
Stand United Vs African Sports
Mgambo Shooting Vs Majimaji Fc
Prisons Vs Mbeya City
Yanga SC Vs JKT Ruvu
Jumapili Sept 20, 2015
Mwadui FC Vs Azam FC
Mtibwa Sugar Vs Ndanda FC
Simba SC Vs Kagera Sugar
Coastal Union Vs Toto Africans
Freddy Felix Minziro amesema anataka pointi tatu kwa Yanga SC kesho Uwanja wa Taifa |
Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
KOCHA wa JKT Ruvu, Freddy Felix Minziro amesema ana hasira za kupoteza mechi mbili za mwanzo za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Nyada za Juu Kusini, hivyo kesho atapambana ashinde mechi ya kwanza.
Baada ya kufungwa 1-0 na Majimaji mjini Songea na 3-0 na Mbeya City mjini Mbeya, JKT Ruvu kesho watacheza mechi ya tatu watakapomenyana na mabingwa watetezi, Yanga SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Na kuelekea mchezo huo, Minziro amesema; “Sisi tayari tumepoteza mechi mbili, japokuwa za ugenini, lakini tumepoteza. Sasa tunahitaji kushinda ili tukae sawa,”amesema.
Kuhusu Yanga SC, Minziro amesema; “Yanga SC ni timu nzuri, lakini ya kawaida tu kama timu nyingine na sisi tutaingia uwanjani kupambana nao bila woga, tunataka pointi tatu,”amesema.
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaendelea wikiendi hii kwa michezo nane kuchezwa Jumamosi na Jumapili katika viwanja nane tofauti nchini ikiwa ni mzunguko wa tatu tangu kuanza kwa ligi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mbali na Yanga na JKT Ruvu, mechi nyingine za Jumamosi ni kati ya Stand United na African Sports Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Mbeya City na Prisons Uwanja wa Sokoine, Mbeya, Mgambo Shooting na Majimaji FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Jumapili Simba SC watawakaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Mwadui FC watakuwa wenyeji wa Azam FC Uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga, Mtibwa Sugar watawakaribisha Ndanda FC ya Mtwara Uwanja wa Manungu, Turiani mjini Morogoro na Coastal Union watakuwa wenyeji wa Toto Africans Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
0 comments:
Post a Comment