// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MICHO AMTEUA WA DARAJA PILI KUIVAA SUDAN KUFUZU CHAN 2017 RWANDA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MICHO AMTEUA WA DARAJA PILI KUIVAA SUDAN KUFUZU CHAN 2017 RWANDA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, September 12, 2015

    MICHO AMTEUA WA DARAJA PILI KUIVAA SUDAN KUFUZU CHAN 2017 RWANDA

    KOCHA wa Uganda, Milutin ‘Micho’ Sredojevic amemteua mchezaji wa Daraja la Pili, Caesar Okhuti (pichani kulia) katika kikosi chake cha wachezaji 25 kwa ajili ya mechi na Sudan kufuzu michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.
    Okuthi ambaye anapambana kujiinua tena kisoka katika Ligi Kubwa ya Shirikisho la Soka Uganda (FUFA) baada ya misimu mitatu migumu akichezea timu ya Daraja la Pili, Onduparaka kwa sasa anachezea Express FC.
    Alihamishiwa Express FC msimu huu na kufunga mabao matatu katika mechi nne, kuwasaidia ‘Tai Wekundu’ wa Kampala kupanda kilalani mwa Ligi Kuu ya Azam Uganda akifunga mabao mawili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Lweza Jumanne.
    Okhuti alikuwa tishio kisoka wakati anaibuka akiwa ana umri wa miaka 18 mwaka 2007 wakati akichezea Edioef Hills FC, lakini akapoteza makali yake.
    Kikosi hicho cha Uganda cha CHAN kinatarajiwa kuanza mazoezi leo Uwanja wa Nakivubo mjini Kampala, kujiandaa kuwakaribisha Sudan Oktoba 17 kabla ya kurudiana mjini Khartoum wiki moja baadaye na mshindi wa jumla atafuzu kwa fainali za CHAN zitakazofanyika Rwanda kuanzia Januari 16 hadi Februari mwaka 2017.
    Micho aliitoa Tanzania kwa jumla ya mabao 3-1 katika Raundi ya Kwanza CHAN

    Kikosi kamili cha Uganda ni; Makipa; Mathias Kigonya (Bright Stars FC), Watenga Isma (Vipers SC) na James Alitho (Vipers SC).
    Mabeki: Denis Okot (KCCA FC), Julius Ntambi (URA FC), Joseph Ochaya (KCCA FC), Aggrey Madoi (Jinja Municipal Hippos FC), Martin Mpuga (KCCA FC), Richard Kasaga (URA FC), Dazo Hassan Wasswa (KCCA FC) na Shafiq Bakaki (Vipers SC)
    Viungo: KezironKizito (Vipers SC), Ivan Ntege (KCCA FC), Deus Bukenya (Vipers), Hakim Senkumba (KCCA FC), Faruku Miya (Vipers SC), Muzamil Mutyaba (KCCA FC), Feni Moses Ali (URA FC) na Martin Kizza (SC Villa Jogoo).
    Washambuliaji: Milton Kalisa (BUL C), Caesar Okhuti (Express FC), Fahad Muhammad Hassan (SC Villa Jogoo), Villa Oromchan (URA FC), John Ssemazi (Vipers SC), Frank Kalanda (URA FC).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MICHO AMTEUA WA DARAJA PILI KUIVAA SUDAN KUFUZU CHAN 2017 RWANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top