WENYEJI Kenya wamefungwa mabao 2-1 na Zambia katika mchezo wa Kundi E Uwanja wa Nyayo, Nairobi kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika.
Kenya walianza vyema baada ya kupata bao la kuongoza kupitia kwa Michael Olunga aliyefunga dakika ya 13, kabla ya Zambia kusawazisha kupitia kwa Winstone Kalengo dakika ya 28.
Bao lililoizima Harambee Stars lilifungwa na mshambuliaji mkongwe wa Chipolopolo, Collins Mbesuma dakika ya 42 na sasa Zambia wanasogea nafasi ya pili kwenye kundi hilo baada ya sare ya 0-0 na Guinea-Bissau katika mchezo wa kwanza Juni.
Kipigo hicho kinaifanya Kenya iangukie nafasi ya tatu katika Kundi E baada ya kutoa sare ya 1-1 na Kongo kwenye mchezo wa kwanza Juni.
Mchezo mwingine wa kundi hilo Kongo imeifunga Guinea-Bissau 4-2 jana.

0 comments:
Post a Comment