MATOKEO MECHI ZA LIGI YA
MABINGWA ULAYA USIKU HUU:
Real Madrid 4 – 0 Shakhtar Donetsk
Manchester City 1 – 2 Juventus
PSV 2 – 1 Manchester United
Galatasaray 0 – 2 Atletico de Madrid
Sevilla 3 – 0 Borussia Monchengladbach
Paris Saint-Germain 2 – 0 Malmo FF
VfL Wolfsburg 1 – 0 CSKA Moscow
Benfica 2 – 0 FC Astana
Real Madrid 4 – 0 Shakhtar Donetsk
Manchester City 1 – 2 Juventus
PSV 2 – 1 Manchester United
Galatasaray 0 – 2 Atletico de Madrid
Sevilla 3 – 0 Borussia Monchengladbach
Paris Saint-Germain 2 – 0 Malmo FF
VfL Wolfsburg 1 – 0 CSKA Moscow
Benfica 2 – 0 FC Astana
Juan Mata akitupa mpira kwa hasira huku Anthony Martial akiwa ameshika uso wake baada ya United kufungwa bao la pili na wenyeji PSV PICHA ZAIDI GONGA HAPA
TIMU za Manchester, England zimeanza vibaya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya zote kuchapwa usiku huu.
Manchester City wakiwa Uwanja wa nyumbani, Etihad wamepigwa 2-1 na Juventus katika mchezo wa Kundi D.
Licha ya City kutangulia bao baada ya Giorgio Chiellini kujifunga dakika ya 57, lakini Mario Mandzukic akasawazisha dakika ya 70 na Alvaro Morata akakifungua bao la ushindi Kibibi Kizee cha Turin dakika ya 81.
Mchezo mwingine wa Kundi D, Sevilla ya Hispania imeanza vyema kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Borussia Monchengladbach ya Ujerumani Uwanja wa Sanchez Pizjuan, mabao yake yakifungwa na Kevin Gameiro dakika ya 47, Ever Banega dakika ya 66 yote kwa penalti na Yevhen Konoplyanka dakika ya 84.
Alvaro Morata (katikati) akishangilia na Juan Cuadrado na Paul Pogba baada ya kuifungia Juventus dhidi ya Man City PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Mashetani Wekundu, Manchester United wameanza vibaya nao japokuwa walikuwa ugenini, baada ya kuchapwa mabao 2-1 na PSV katika mchezo wa Kundi B Uwanja wa Philips.
United pia walitangulia kupata bao, mchezaji wake mpya Memphis Depay akiiadhibu timu yake ya zamani dakika ya 41, kabla ya Hector Moreno kusawazisha dakika ya 47 na Luciano Narsingh kufunga la pili dakika ya 57.
Mchezo mwingine wa Kundi B, VfL Wolfsburg ya Ujerumani imepata ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya CSKA Moscow ya Urusi, bao pekee la Julian Draxler dakika ya 40 Uwanja wa Volkswagen Arena.
Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia mabao matatu Real Madrid ikishinda 4-0 dhidi ya Shakhtar PICHA ZAIDI GONGA
Kundi C, Atletico Madrid wameanza vyema kwa ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya Galatasaray nchini Uturuki, mabao ya Antoine Griezmann dakika ya 18 na 25 Uwanja wa Turk Telekom Arena, wakati Benfica ya Ureno imeshinda 2-0 nyumbani dhidi ya FC Astana, mabao ya Nicolas Gaitan dakika ya 51 na Kostas Mitroglou dakika ya 62 Uwanja wa
da Luz.
Kundi A; Paris Saint-Germain wameanza vyema pia kwa ushindi wa 2-0 nyumbani dhidi ya Malmo FF, mabao ya Angel Di Maria dakika ya nne na Edinson Cavani dakika ya 61 Uwanja wa Parc des Princes.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, Real Madrid wameifumua mabao 4-0 Shakhtar Donetsk Uwanja wa Bernabeu, Mwanasoka Bora wa Dunia, Crisitano Ronaldo akifunga matatu peke yake, dakika za 54, 63 yote kwa penalti na 81, wakati lingine likifungwa na Mfaransa Karim Benzema dakika ya 30.
Winga wa zamani wa Real Madrid na Manchester United, Angel Di Maria akishangilia baada ya kuifungia PSG PICHA ZAIDI GONGA HAPA
MECHI ZA JUMATANO;
Hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itaendelea leo kwenye viwanja nane, Valencia CFikiikaribisha Zenit St Petersburg Uwanja wa Mestalla, Roma ikiikaribisha Barcelona Uwanja wa Olimpico, Olympiakos ikiikaribisha FC Bayern Munich Uwanja wa Georgios Karaiskakis, KAA Gent ikiikaribisha Lyon Uwanja wa Ghelamco, Dynamo Kyiv ikiikaribisha FC Porto Uwanja wa Kiev Olympic, Dinamo Zagreb ikiikaribisha Arsenal Uwanja wa Maksimir, Chelsea ikiwakaribisha Maccabi Tel Aviv Uwanja wa Stamford Bridge na Bayer 04 Leverkusen ikiwakaribisha BATE Borisov Uwanja wa BayArena.
0 comments:
Post a Comment