Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
KLABU ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini imevutiwa na wachezaji vijana wadogo watano wa Kitanzania na sasa inafanya mpango wa kuwachukua kuwaendeleza kisoka.
Wachezaji wa timu ya vijana ya taifa chini ya umri wa miaka 15, Athumani Maulid, Kelvin Deogratius, Maziku Amani, Asad Juma na Issa Makamba walikuwa Pretoria, Afrika Kusini tangu mwishoni mwa Agosti hadi mwanzoni mwa mwezi huu kwa majaribio.
Na wachezaji hao ambao waliongozana na Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Madadi imeelezwa wamefanya vizuri.
Rais wa TFF, Jamal Emil Malinzi ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE jana kwamba, amepewa taarifa kutoka Pirates kwamba vijana wamefanya vizuri na anasubiri hatua zaidi.
Wachezaji waliozufu majaribio Orlando Pirates, Juu kutoka kulia ni Kelvin Deogratius, Athumani Maulid na Maziku Amani. Chini ni Asad Juma kushoto na Issa Makamba kulia.
“Lengo ni vijana waende kule kucheza kukusanya ujuzi na uzoefu zaidi, ili baadaye waje kulisaidia taifa. Alinipigia rafiki yangu Irvin Khoza (Rais wa Pirates) akawasifu sana wale vijana. Akasema anaandaa taratibu za kuwaita wakaanze kucheza kule kikosi cha U20 ya Pirates,”amesema Malinzi.
Rais huyo wa TFF, aliyepania kuiinua soka ya Tanzania amesema huo ni mwanzo tu, kwani anafanya jitihada zaidi kuhakikisha vijana wadogo wengi wanapata nafasi ya kujiunga na timu za vijana nje hadi za Ulaya.
Tayari Malinzi anaendelea na mkakati madhubuti wa kuunda timu bora ya vijana kwa ajili ya Fainali za Vijana Afrika mwaka 2019, ambazo Tanzania inaweza kuwa mwenyeji.
Juni mwaka huu TFF ilifanya mashidano ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 13 mjini Mwanza na japo la makocha chini ya Idara ya ufundi ya TFF ikachagua vijana wenye vipaji ambao kuunda timu ya taifa ya U13.
Sasa vijana hao wamepelekwa shule ya Alliance mjini Mwanza kuendelezwa kisoka na elimu- baada ya TFF kuingia mkataba na shule hiyo maarufu kwa kuzalisha vipaji.
Mpango huo utaendelea na mwakani kwa kuchagua vijana wenye umri chini ya miaka 14 (U14), na mwaka unaofuata kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15) kwa lengo la kuendelea kuboresha kikosi hicho cha vijana ili kupata U17 bora kwa ajili ya 2019.
Wachezaji wa U13 waliochaguliwa kujiunga na timu hiyo ni Jaffar Juma (Arusha), Moris Michael (Ilala - Dsm), Jonathan Raphael (Kasulu – Kigoma), Karim Mfaume (Lindi), Erick Buyaga (Nyamagana – Mwanza), Shabani Kimwaga (Kinondoni – Dsm), Feisally Awadh (Ilala – Dsm), Abdulatif Noor (Tanga), Edmond Godfrey (Geita) na Adam Selemani (Kibaha – Pwani).
Wengine ni Selaman Juma (Kibaha – Pwani), Wilbert John (Ilala – Dsm), Ahsante Hamisi (Kinondoni – Dsm), Isaya Ernest (Mbeya), Gasper Gombanila (Nyamagana – Mwanza), Joseph Awadh (Ilala – Dsm), Alfonsi Mabula (Nyamagana - Dsm), Cosmas Lucas (Nyamagana – Mwanza), Haroub Juma (Bariadi – Simiyu) na Ladak Juma (Morogoro).

0 comments:
Post a Comment