TIMU ya taifa ya Kenya imetoka nyuma na kuifunga Cameroon 3-1 jana katika fainali ya mpira wa wavu na kutwaa Medali ya Dhahabu mjin Brazaville, Kongo.
Cameroon ilielekea kuifunga mara ya pili ya Kenya katika Michezo ya mwaka huu, baada ya kuongoza seti ya kwanza.
Hata hivyo, kilichotokea katika mchezo wa kwanza hakikujirudia safari hii, baada ya Kenya kushinda seti tatu zilizofuata.
Kocha Paul Gitau alikuwa mwenye furaha kutokana na ushindi huo na akasema; “Nilisema hapa, ikiwa tutaongoza Kundi tutakwenda moja kwa moja kubeba Medali ya Dhahabu. Nina furaha tumethibitisha hilo kwamba sisi ni bora,”.
Misri imeifunga Shelisheli 3-0 na kubeba Medali ya Shaba.
Kenya ambayo ilikuwa na wachezaji chipukizi, kutokana na timu ya wakubwa kuwa Japan kwenye michuano ya Dunia wakati Michezo ya Afrika inaanza, haikutarajiwa kufanya vizuri Kongo.
Lakini licha kufungwa 3-2 na Cameroon katika mchezo wao wa tatu wa kundi baada ya kuongoza kwa 2-0, Kenya ilizinduka na kuzifunga Algeria na Nigeria katika hatua ya makundi, kabla ya kuifunga na Misri katika Nusu fainali.
Cameroon nayo ilijipigia kiulaini Shelisheli katika Nusu Fainali nyingine na kukutana na Wakenya fainali.

0 comments:
Post a Comment