// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); LIVERPOOL YAANZA KWA SARE EUROPA LEAGUE, SPURS YAWACHAPA 3-1 FK QARABAG - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE LIVERPOOL YAANZA KWA SARE EUROPA LEAGUE, SPURS YAWACHAPA 3-1 FK QARABAG - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, September 18, 2015

    LIVERPOOL YAANZA KWA SARE EUROPA LEAGUE, SPURS YAWACHAPA 3-1 FK QARABAG

    MATOKEO MECHI ZA JANA UEFA EUROPA LEAGUE 
    Asteras Tripolis 1 - 1 Sparta Prague 
    APOEL Nicosia 0 - 3 FC Schalke 04 
    Dnipro Dnipropetrovsk 1 - 1 Lazio 
    Sporting Lisbon 1 - 3 Lokomotiv Moscow 
    Skenderbeu Korce 0 - 1 Besiktas
    Fiorentina  1 - 2 FC Basel
    Tottenham Hotspur 3 - 1 FK Qarabag
    Athletic Club 3 - 1 FC Augsburg
    Lech Poznan 0 - 0 Belenenses
    Partizan Belgrade 3 - 2 AZ
    Ajax 2 - 2 Celtic
    Viktoria Plzen 2 - 0 Dinamo Minsk
    Napoli 5 - 0 Club Brugge
    Bordeaux  1 - 1 Liverpool
    FK Qabala 0 - 0 PAOK Salonika
    FC Sion 2 - 1 Rubin Kazan
    Slovan Liberec  0 - 1 Sporting Braga
    SK Rapid Wien 2 - 1 Villarreal
    Borussia Dortmund 2 - 1 FK Krasnodar
    FC Groningen 0 - 3 Marseille
    Fenerbahce 1 - 3 Molde
    FC Midtjylland 1 - 0  Legia Warsaw
    Kiungo wa Liverpool, Adam Lallana (kushoto) akipambana na Nicolas Maurice-Belay wa Bordeaux (kulia) katika mchezo wa Europa League jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    LIVERPOOL wamelazimisha sare ya 1-1 na Bordeaux ugenini katika mchezo wa Kundi B UEFA Europa League usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Matmut Atlantique, Ufaransa.
    Adam Lallana alianza kuifungia Liverpool mjini Bordeaux dakika ya 65, kabla ya Jussie Ferreira Vieira kusawazishia wenyeji dakika ya 81.
    Timu nyingine ya England, Tottenham Hotspur imeanza vyema kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya FK Qarabag mchezo wa Kundi J Uwanja wa White Hart Lane, London, mabao yake yakifungwa na Heung-Min Son dakika ya 28 na 30 na Erik Lamela dakika ya 86, huku wageni wakipata bao lao kwa penalti dakika ya saba kupitia kwa Richard Almeida.Fenerbahce striker Robin Van Persie was unable to add to his single goal since joining from United
    Mshambuliaji wa Fenerbahce, Robin Van Persie alishindwa kufunga jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    Mchezo mwingine wa kundi hilo, RSC Anderlecht imetoa sare ya 1-1 na Monaco bao likifungwa Guillaume Gillet dakika ya 11, kabla ya Lacina Traore kusawazisha dakika ya 85 Uwanja wa Constant Vanden Stockstadion.
    Kundi K, FC Schalke ya Ujerumani imeshinda 3-0 ugenini dhidi ya APOEL Nicosia Uwanja wa GSP nchini Cyprus mabao ya Joel Matip dakika ya 28 na Klaas-Jan Huntelaar dakika ya 35 na 71.
    Lazio imelazimisha sare ya 1-1 ugenini na Dnipro Dnipropetrovsk  katika mchezo wa Kundi G, bao lao likifungwa na Sergej Milinkovic-Savic dakika ya 34 kabla ya wenyeji kusawazisha dakika ya 90 na ushei kupitia kwa Evgen Seleznyov Uwanja wa Dnipro Arena.
    Monaco 
    Fiorentina imechapwa 2-1 katika mchezo wa Kundi I na FC Basel licha ya kuongoza kwa 1-0 hadi mapumziko kwa bao la Nikola Kalinic dakika ya tatu, kwani kipindi cha pili Birkir Bjarnason aliwasawazishia ugenini ya 71 na Mohamed Elneny akafunga la ushindi dakika ya 79 Uwanja wa Artemio Franchi.
    Tottenham head coach Mauricio Pochettino opted to ring the changes for his side's Europa League opener with Qarabag 
    Kikosi cha Tottenham kilichoiadhibu Qarabag jana  PICHA ZAIDI GONGA HAPA
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIVERPOOL YAANZA KWA SARE EUROPA LEAGUE, SPURS YAWACHAPA 3-1 FK QARABAG Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top