// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); LIGI DARAJA LA KWANZA YAANZA KESHO, RANGERS NA MAAFANDE KAZI IPO MLANDIZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE LIGI DARAJA LA KWANZA YAANZA KESHO, RANGERS NA MAAFANDE KAZI IPO MLANDIZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, September 18, 2015

    LIGI DARAJA LA KWANZA YAANZA KESHO, RANGERS NA MAAFANDE KAZI IPO MLANDIZI

    MECHI ZA UFUNGUZI LIGI DARAJA LA KWANZA KESHO;
    Kundi A;
    Polisi Dar Vs Friends Rangers (Mabatini, Mlandizi)
    Mjii Mkuu Vs  Polisi Dodoma (Jamhuri, Dodoma)
    Kundi B;
    Polisi Moro Vs Burkina Faso (Jamhuri Morogoro)
    Mji Njombe FC Vs Kurugenzi (Amani, Njombe)
    Lipuli FC Vs Kimondo FC (Wambi, Iringa)
    JKT Mlale Vs Ruvu Shooting (Majimaji, Songea) 
    Kundi C;
    Mbao FC Vs Geita Gold (CCM Kirumba, Mwanza)
    Rhino Rangers Vs Polisi Tabora (A.H. Mwinyi  Tabora)
    Panone FC Vs JKT Oljoro (Ushirika, Moshi)
    Polisi Mara Vs JKT Kanembwa (Karume, Mara).
    Friends Rangers wataanza na Polisi Dar es Salaam kesho Mlandizi

    LIGI Daraja la Kwanza nchini (FDL) inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho Jumamosi Septemba 19 kwa michezo 10 kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini, ambapo jumla ya timu 24 zinashirki ligi hiyo zitaanza kusaka nafasi tatu za juu ili kuweza kupanda Ligi Kuu msimu ujao.
    Kundi A, Polisi Dar watakuwa wenyeji wa Friends Rangers kwenye uwanja Mabatini mkoani Pwani, Mjii Mkuu ya Dodoma watapambana na  Polisi Dodoma kwenye uwanja wa Jamhuri mjini humo.
    Kundi B, Polisi Morogoro watacheza na Burkina Faso uwanja wa Jamhuri Morogoro, Njombe Mji FC watacheza na Kurugenzi uwanja wa Amani mjini Njombe, Lipuli ya Iringa watawaribisha Kimondo FC uwanja wa Wambi- Iringa na JKT Mlale watakua wenyeji wa Ruvu Shooting katika uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma.
    Kundi C, Mbao FC watawakaribisha Geita Gold uwanja wa CCM Kirumba, Rhino Rangers watacheza dhidi ya Polisi Tabora uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, Panone FC watawakaribisha JKT Oljoro katika uwanja wa Ushirka mjini Moshi na Polisi Mara watakua wenyeji wa JKT Kanembwa kwenye uwanja wa Karume mkoani Mara.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIGI DARAJA LA KWANZA YAANZA KESHO, RANGERS NA MAAFANDE KAZI IPO MLANDIZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top