// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KUMEKUCHA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA, MAMBO YATAANZA HIVI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KUMEKUCHA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA, MAMBO YATAANZA HIVI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, September 08, 2015

    KUMEKUCHA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA, MAMBO YATAANZA HIVI



    RATIBA YA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA 

    Septemba 12, 2015
    Ndanda FC Vs Mgambo JKT
    African Sports Vs Simba SC
    Majimaji FC Vs JKT Ruvu
    Azam FC Vs Prisons
    Stand United Vs Mtibwa Sugar
    Toto Africans Vs Mwadui
    Mbeya City Vs Kagera Sugar
    Septemba 13, 2015
    Yanga SC Vs Coastal Union
    Septemba 16, 2015
    Yanga SC Vs Prisons
    Mgambo JKT Vs Simba SC
    Majimaji FC Vs Kagera Sugar
    Mbeya City Vs JKT Ruvu
    Stand United Vs Azam FC
    Toto Africans Vs Mtibwa Sugar
    Ndanda FC Vs Coastal Union
    Septemba 17, 2015
    Mwadui FC Vs African Sports
    Septemba 19, 2015
    Stand United Vs African Sports
    Mgambo JKT Vs Majimaji FC
    Prisons Vs Mbeya City
    Yanga SC Vs JKT Ruvu
    Septemba 20, 2015
    Mwadui FC Vs Azam FC
    Mtibwa Sugar Vs Ndanda FC
    Simba SC Vs Kagera Sugar
    Coastal Union Vs Toto Africans
    Septemba 26, 2015
    Simba SC Vs Yanga SC
    Coastal Union Vs Mwadui FC
    Prisons Vs Mgambo JKT
    JKT Ruvu Vs Stand United
    Mtibwa Sugar Vs Majimaji FC
    Kagera Sugar Vs Toto Africans
    Septemba 27, 2015
    African Sports Vs Ndanda FC
    Azam FC Vs Mbeya City
    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    LIGIi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2015/2016 inatazamiwa kuanza kutimua vumbi jumamosi Septemba 12, 2015 kwa michezo saba kuchezwa katika viwanja tofauti nchini.
    Ndanda FC ya Mtwara watakua wenyeji wa Mgambo Shooting katika uwanja wa Nagwanda Sijaona mjini Mtwara, Wana kimanumanu African Sports watawakaribisha Simba SC katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, huku Wana Lizombe Majimaji wakiwa wenyeji wa maafande wa JKT Ruvu katika uwanja wa Majimaji mjini Songea.
    Azam FC watakua wenyeji wa Tanzania Prisons kaika uwanja wa Chamazi Complex, Stand United FC chama la wana watawakaribisha Mtibwa Sugar katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Toto Africans watawakaribisha Mwadui FC uwanja wa CCM Kirumba na Mbeya City watacheza na Kagera Sugar katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
    Jumapili Ligi Kuu itaendelea kwa mchezo mmoja tu utakaochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ambapo mabingwa watetezi wa kombe hilo Yanga SC watawakribisha wagosi wa kaya Coastal Union.
    Katika hatua nyingine klabu ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera itatumia  Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora kwa mechi zake za nyumbani dhidi ya Toto Africans (Sept 26), JKT Ruvu (Sept 30), Tanzania Prisons (Oct 4) na Yanga (Oct 31).
    Mabadiliko hayo yamefanyika kupisha shughuli ya uwekaji nyasi bandia inayoendelea kwenye uwanja wao wa Kaitaba mjini Bukoba unaofanywa na wataalamu kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KUMEKUCHA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA, MAMBO YATAANZA HIVI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top