NAHODHA wa Nigeria na kipa tegemeo, Vincent Enyeama (pichani) ameenguliwa kwenye kikosi kitakachoivaa Tanzania Jumamosi katika mchezo wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika.
Chanzo cha habari kimesema kipa huyo wa Super Eagles mwenye umri wa miaka 33 anayedakia Lille OSC ya Ufarana ameomba mwenyewe kuondolewa na msafara unaokuja Dar es Salaam kutokana na mambo binafsi yakiwemo ya kifamilia.
"Vincent alitarajiwa kuwasili Abuja katika kambi ya Super Eagles jana (Jumanne) lakini ameoiga simu kuomba kuondolewa kwenye kikosi kitakachomenyana na Tanzania kutokana na matatizo ya kifamiia.
"Sasa timu itasafiri na makipa wawili waliopo kambini kwa sasa, labda kocha aamue kuita kipa mwingine jambo ambalo nina wasiwasi haliwezekani,"kimesema chanzo.
Mzigo wa kudaka mechi dhidi ya Taifa Stars sasa unaangukia kwa kipa wa Wolves, Carl Ikeme au Ikechukwu Ezenwa wa Sunshine Stars.
Nigeria ilianza vyema kampeni zao za kufuzu AFCON ya 2017 kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Chad mwezi Juni, wakati Tanzania ilianza vibaya kwa kufungwa 3-0 na Misri.

0 comments:
Post a Comment