Na Princess Asia, TANGA
MFUNGAJI wa bao pekee la Simba SC katika mchezo wa dhidi ya African Sports ya Tanga, Hamisi Kiiza, amesema kwamba anamshukuru Mungu kwa kuitikia dua zake.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda, ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE leo mjini hapa kwamba alikuwa akiomba Mungu kuhakikisha anaisaidia timu yake ya Simba kushinda kwa sababu anaamini baada ya kufanya mazoezi kila mmoja anatarajia kupata ushindi.
" Asante sana Mungu kwa kunisaidia leo kufunga, ninafuraha kwa kupata ushindi huu, nawapongeza wachezaji wenzangu pia kwa kuonyesha juhudi, nawashukuru pia mashabiki kwa umoja wao," amesema Kiiza.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga SC, ameongeza kwamba katika ligi hakuna mechi nyepesi na kazi ya wachezaji ni kujituma uwanjani kuhakikisha wanapata ushindi ili waweze kutimiza malengo ya kuchukua ubingwa.
Kiiza alisajiliwa na Simba akiwa ni mchezaji huru baada ya kuchwa na Yanga na kukaa mwaka mzima bila ya kuwa na klabu huku mipango ya kujiunga na Fanja ya Oman ikikwama.

Hamisi Kiiza amesema Mungu amesikia dua zake SImba SC |
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga SC, ameongeza kwamba katika ligi hakuna mechi nyepesi na kazi ya wachezaji ni kujituma uwanjani kuhakikisha wanapata ushindi ili waweze kutimiza malengo ya kuchukua ubingwa.
Kiiza alisajiliwa na Simba akiwa ni mchezaji huru baada ya kuchwa na Yanga na kukaa mwaka mzima bila ya kuwa na klabu huku mipango ya kujiunga na Fanja ya Oman ikikwama.
0 comments:
Post a Comment