Na Princess Asia, TANGA
KOCHA wa Simba SC, Muingereza Dylan Kerr amesema ana matumaini wachezaji wake majeruhi, Hassan Isihaka na Ibrahim Hajib watakuwa fiti kwa ajili ya mchezo na Mgambo JKT Jumatano.
Simba SC iliwakosa wawili hao pamoja na viungo Abdi Banda na Jonas Mkude katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jana dhidi ya African Sports Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji wao hao jana, Wekundu wa Msimbazi watashuka tena dimba la Mkwakwani Jumatano kumenyana na Mgambo JKT katika mfululizo wa LIgi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Na Kerr amesema maumivu ya Isihaka na Hajib hayatakuwa ya muda mrefu, hivyo ana matumaini ya kuwa nao mazoezini kuanzia kesho.
“Isihaka na Hajib sitarajii kuendelea kuwakosa, natumai nitakuwa nao mazoezini kuanzia Jumatatu,”amesema Kerr ambaye alianza kazi Simba SC Julai mwaka huu akirithi mikoba ya Mserbia, Goran Kopunovic.
Wachezaji wa Simba SC wamepewa mapumziko leo baada ya ushindi wa jana wa bao la Mganda Hamisi Kiiza ‘Diego’ na kesho wanatarajiwa kuendelea na mazoezi mjini Tanga.

Dylan Kerr alianza vizuri Ligi Kuu jana kwa ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Sports Uwanja wa Mkwakwani, Tanga |
Na Kerr amesema maumivu ya Isihaka na Hajib hayatakuwa ya muda mrefu, hivyo ana matumaini ya kuwa nao mazoezini kuanzia kesho.
“Isihaka na Hajib sitarajii kuendelea kuwakosa, natumai nitakuwa nao mazoezini kuanzia Jumatatu,”amesema Kerr ambaye alianza kazi Simba SC Julai mwaka huu akirithi mikoba ya Mserbia, Goran Kopunovic.
Wachezaji wa Simba SC wamepewa mapumziko leo baada ya ushindi wa jana wa bao la Mganda Hamisi Kiiza ‘Diego’ na kesho wanatarajiwa kuendelea na mazoezi mjini Tanga.
0 comments:
Post a Comment