TIMU ya Inter Milan imewafunga mahasimu AC Milan 1-0 na kupanda kileleni mwa Serie A jana, huku mshambuliaji Mario Balotelli akikosa mabao ya wazi baada ya kutokea benchi kucheza dhidi ya timu yake ya zamani, The Rossoneri.
Fredy Guarin alisherehekea mechi yake ya 100 ya ligi kwa kufunga bao pekee la ushindi dakika ya 58 baada ya kupoteza nafasi kadhaa.
Balotelli, ambaye ambaye amerejea Milan kwa mkopo kutoka Liverpool mwezi uliopita aligongesha mwamba nma baadaye akakaribia kufunga kwa mpira wa adhabu, kabla ya kuzinguana na Filipe Melo wa Inter.
Balotelli alianzia Inter kabla ya kuhamia Manchester City mwaka 2010 na jana alitokea benchi kwenda kucheza dhidi ya timu iliyomuibua ambayo mashabiki wake walimzomea jana.
Kikosi cha Inter Milan kilikuwa; Handanovic, Santon, Medel, Murillo, Nunes Jesus/Telles dk68, Guarin, Felipe Melo, Kondogbia, Perisic/Ranocchia dk85, Icardi na Jovetic/Palacio dk72.
Ac Milan; Lopez, Abate, Zapata, Romagnoli, De Sciglio, Kucka/Poli dk72, Montolivo, Bonaventura, Honda/Cerci dk81, Luiz Adriano na Bacca/Balotelli dk62.
0 comments:
Post a Comment