NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA
Septemba 25, 2015
ES Sahel (Tunisia) Vs Zamalek
Septemba 26, 2015
Orlando Pirates Vs Al Ahly (Misri)
Oktoba 2, 2015
Zamalek (Misri) Vs ES Sahel (Tunisia)
Oktoba 3, 2015
Al Ahly (Misri) Vs Orlando Pirates
Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Mrisho Ngassa akiwania mpira dhidi ya beki wa Etoile du Sahel ya Tunisia, Boughattas Zied katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika Aprili 18, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka 1-1 kabla ya Yanga kwenda kufungwa 1-0 mchezo wa marudiano na kutolewa.
Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
YANGA SC walitolewa katika hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kufungwa kwa jumla ya mabao 2-1 na Etoile du Sahel ya Tunisia.
Mchezo wa kwanza Dar es Salaam timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1 na marudiano mjini Sousse, Yanga SC ilifungwa 1-0 kwa mbinde na Waarabu hao.
Yanga SC ilirudi nyumbani na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Mei mwaka huu na sasa wanaifikiria Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
Lakini ES Sahel imeendelea vyema na safari yake katika michuano hiyo ya pili kwa ukubwa barani na sasa imetinga Nusu Fainali.
ES Sahel imefungana kwa pointi na Al Ahly ya Misri kileleni mwa Kundi A, kila timu ikimaliza na pointi 13, hivyo zote kwenda Nusu Fainali, zikizipiku Stade Malien ya Mali na Esperane ya Tunisia.
Sasa Ahly iliyoizidi kwa wastani wa mabao ES Sahel itamenyana na Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho, wakati wababe wa Yanga watamenyana na Zamalek ya Misri.
Mechi za kwanza zitachezwa mwishoni mwa mwezi huu, wakati marudiano yatakuwa mapema mwezi ujao.
Na hata mwaka jana, Yanga SC ilitolewa na Al Ahly ya Misri katika hatua za awali za Ligi ya Mabingwa Afrika. Ahly ikaenda kutolewa katika 16 Bora na kuangukia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
Ikashinda na kuingia kwenye makundi ambako ilishinda mechi zote hadi kutwaa Kombe hilo- ambalo sasa inawania kulitetea.
Bila shaka, Yanga SC wana kila sababu ya kujifariji kwamba walisogea mbali kidogo katika michuano ya Afrika mwaka huu baada ya kuzitoa BDF ya Botswana na Platinum ya Zimbabwe kabla ya kutolewa na ES Sahel ambayo sasa inaelekea kuwa bingwa wa Kombe hilo.

Etoile du Sahel wakiwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Aprili mwaka huu kabla ya mechi na Yanga SC. Wanaume hao wamekaribia kutwaa Kombe la Shirikisho |
Na hata mwaka jana, Yanga SC ilitolewa na Al Ahly ya Misri katika hatua za awali za Ligi ya Mabingwa Afrika. Ahly ikaenda kutolewa katika 16 Bora na kuangukia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
Ikashinda na kuingia kwenye makundi ambako ilishinda mechi zote hadi kutwaa Kombe hilo- ambalo sasa inawania kulitetea.
Bila shaka, Yanga SC wana kila sababu ya kujifariji kwamba walisogea mbali kidogo katika michuano ya Afrika mwaka huu baada ya kuzitoa BDF ya Botswana na Platinum ya Zimbabwe kabla ya kutolewa na ES Sahel ambayo sasa inaelekea kuwa bingwa wa Kombe hilo.
0 comments:
Post a Comment