AGOSTI 20, mwaka huu Chelsea ilikamilisha usajili wa kiungo Pedro Eliezer Rodriguez Ledesma maarufu tu kama Pedro akijiunga na mabingwa hao wa England kwa dau la Pauni Milioni 19 ambalo litapanda hadi Pauni Milioni 21.4
Siku tatu tu baadaye, mchezaji huyo kutoka Barcelona akacheza mechi yake ya kwanza, Chelsea ikiifunga 3-2 West Bromwich Albion ugenini huku Pedro pia akifunga bao lake la kwanza na kutoa pasi ya bao lililofungwa na mchezaji mwenzake wa Hispania, Diego Costa.
Nchini Tanzania, klabu kadhaa zimefanya usajili wa wachezaji wapya wakiwemo wa kigeni na klabu tatu kubwa Azam FC, SImba na Yanga SC zilitoa maelfu ya dola kusajili.
Hadi sasa mchezaji anayetajwa kusajiliwa kwa gharama kubwa upande wa Yanga SC ni beki Vincent Bossou kutoka Togo, ambaye alikuwa anacheza Korea.
Inadaiwa, Bossou amesajiliwa kwa dola za Kimarekani 100,000 zaidi ya Sh. Milioni 200 za Tanzania ili kumarisha ukuta wa wana Jangwani hao.
Upande wa Azam FC inadaiwa mshambuliaji Mkenya, Alan Wanga amegharimu zaidi ya dola 100,000 katika usajili wake wakati Simba SC baada ya kumkosa Mrundi, Kevin Ndayisenga ambaye ilikuwa tayari kutumia dola 30,000 (Sh. Milioni 90) ikamsajili Msenegal, Pape Abdoulaye N’daw.
Wanga alicheza mechi ya kwanza Azam FC ikishinda 2-1 dhidi ya Prisons Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, wakati N’daw na Bossou wote hawakucheza mechi za kwanza za Ligi Kuu.
Sababu ni nini? Wanajua wenyewe viongozi na makocha wa Simba na Yanga SC, lakini sisi wa nje tunaweza kusema tu hawawaamini wachezaji hao.
Bossou yupo nchini tangu mwezi uliopita na alikuwepo kwenye kambi ya Tukuyu mkoani Mbeya kujiandaa na mchezo wa Ngao Jamii dhidi ya Azam FC.
Alitumiwa kwa dakika 45 tu za kwanza katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Mbeya City Yanga SC ikishinda 3-2 Uwanja wa Sokoine.
Akamalizia benchi dakika zote 90 mchezo wa Ngao ya Jamii, Yanga SC ikishinda kwa penalti 8-7 dhidi ya Azam FC.
Baada ya hapo Yanga SC imerudi kambini kujiandaa na Ligi Kuu kabla ya mwishoni mwa wiki kuibuka na kushinda 2-0 dhidi ya Coastal Union, siku hiyo pia Bossou hakucheza.
N’daw naye alicheza karibu mechi zote za kirafiki za Simba SC katika kambi ya Zanzibar na kutocheza kwake Jumamosi dhidi ya African Sports kocha Dylan Kerr anajua.
Mashabiki wa Simba SC wamekwishamuona N’daw akiichezea Simba SC, lakini wa Yanga SC walimuona kwa dakika 45 Bossou- lazima watakuwa wanatamani kumuona tena.
Lakini pia mchezaji anayesajiliwa kwa bei kubwa maana yake ni muhimu kwa mahitaji ya timu- haiwezekani mchezaji wa aina hiyo asiwe na nafasi kwenye kikosi cha kwanza.
Tunaona wenzetu dunia nzima hususan Ulaya, kocha anapoamua kusajili mchezaji wa gharama kubwa, basi ameona umuhimu wa kufanya hivyo na mchezaji huyo anapoingia katika timu anakwenda kucheza moja kwa moja.
Nimetoa mfano wa Pedro kwa sababu ni mchezaji aliyesajiliwa msimu huu na tulimuona siku tatu baadaye akianza katika kikosi cha kwanza cha Chelsea- lakini hiyo ni dunia nzima.
Utaratibu wa kusajili mchezaji ghali na kwenda kumuweka benchi ni wa hapa hapa Tanzania.

0 comments:
Post a Comment