Na Princess Asia, TANGA
MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amempongeza Hamisi Friday Kiiza kwa kufunga katika mechi mbili mfululizo, lakini amemuambia; “Usivimbe kichwa”.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE jioni ya leo Uwanja wa Mkwakwani, Tanga baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya JKT Mgambo, Poppe amesema wamefurahi kuondoka na pointi sita Tanga.
“Tanga ni kugumu, wengi wanajua. Kuvuna pointi sita mapema tu hapa, hakika huu ni mwanzo mzuri. Nawapongeza wachezaji na benchi la Ufundi kwa umoja wao ulioleta matunda haya,”amesema.
Aidha, Poppe amempongeza Mganda Kiiza kwa kucheza katika kiwango kizuri kwenye mechi mbili mfululizo na kufunga mabao mara zote.
“Kwa kweli Kiiza sisi tunajua ni mchezaji mzuri tangu yupo Yanga, ndiyo maana tulimsajili. Nachukua fursa hii pia kumpongeza yeye binafsi, lakini namsihi asivimbe kichwa. Aendelee kuwa mchezaji mwenye nidhamu na ashirikiane na wenzake,”amesema Poppe.
“Ushindi unatokana na umoja na ushirikiano wa wachezaji uwanjani kwa kufuata maelekezo ya kocha. Tunacheza kuanzia nyuma tukitafuta namna ya kwenda kutumbukiza mpira kwenye lango la wapinzani. Hadi mpira unamfikia mfungaji, basi umepita kwenye miguu ya wachezaji wengi. Sasa asitokee mtu mmoja akajiona zaidi ya wenzake, wote ni sawa,”amesema Poppe.
“Kikubwa ninaomba mshikamano huu uendelee ili timu ili iendelee kushinda. Lengo mwaka huu ni kuchukua ubingwa,”ameongeza Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Simba SC imetimiza pointi sita katika Ligi Kuu leo baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mgambo Uwanja wa Mkwakwani - siku tano tu tangu iifunge 1-0 African Sports hapa hapa Tanga.
Simba SC wanarejea Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu, watakapomenyana na Kagera Sugar ya Bukoba Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kabla ya kukutana na mahasimu wao, Simba SC Septemba 26.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe leo Mkwakwani, Tanga |
Hamisi Kiiza kulia akishangilia baada ya kufunga bao la pili leo Uwanja wa Mkwakwani |
“Kwa kweli Kiiza sisi tunajua ni mchezaji mzuri tangu yupo Yanga, ndiyo maana tulimsajili. Nachukua fursa hii pia kumpongeza yeye binafsi, lakini namsihi asivimbe kichwa. Aendelee kuwa mchezaji mwenye nidhamu na ashirikiane na wenzake,”amesema Poppe.
“Ushindi unatokana na umoja na ushirikiano wa wachezaji uwanjani kwa kufuata maelekezo ya kocha. Tunacheza kuanzia nyuma tukitafuta namna ya kwenda kutumbukiza mpira kwenye lango la wapinzani. Hadi mpira unamfikia mfungaji, basi umepita kwenye miguu ya wachezaji wengi. Sasa asitokee mtu mmoja akajiona zaidi ya wenzake, wote ni sawa,”amesema Poppe.
“Kikubwa ninaomba mshikamano huu uendelee ili timu ili iendelee kushinda. Lengo mwaka huu ni kuchukua ubingwa,”ameongeza Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Simba SC imetimiza pointi sita katika Ligi Kuu leo baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mgambo Uwanja wa Mkwakwani - siku tano tu tangu iifunge 1-0 African Sports hapa hapa Tanga.
Simba SC wanarejea Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu, watakapomenyana na Kagera Sugar ya Bukoba Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kabla ya kukutana na mahasimu wao, Simba SC Septemba 26.
0 comments:
Post a Comment