// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ENGLAND YAFUZU EURO 2016, WALCOTT APIGA MBILI ‘SIMBA WATATU’ WAKIUA 6-0 SAN MARINO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ENGLAND YAFUZU EURO 2016, WALCOTT APIGA MBILI ‘SIMBA WATATU’ WAKIUA 6-0 SAN MARINO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, September 06, 2015

    ENGLAND YAFUZU EURO 2016, WALCOTT APIGA MBILI ‘SIMBA WATATU’ WAKIUA 6-0 SAN MARINO

    Nahodha wa England, Wayne Rooney akiinua mikono juu kushangilia baada ya kufunga bao la kwanza kwa penalti Uwanja wa Olimpiki mjini Serravalle na kuihakikishia nchi yake tiketi ya Euro 2016  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    MECHI ZILIZOBAKI KUNDI E KUFUZU EURO 2016

    Septemba 5
    Uswisi vs Slovenia
    Septemba 8 
    England vs Uswisi, Lithuania vs San Marino, Slovenia vs San Marino
    Oktoba 9 
    England vs Estonia, Slovenia vs Lithuania, Uswisi vs San Marino
    Oktoba 12 
    Estonia vs Uswisi, 
    Lithuania vs England, 
    San Marino vs Slovenia 
    TIMU ya taifa ya England imejihakikishia kucheza Fainali za Mataifa ya Ulaya, baadaye mwaka huu, baada ya kuwafunga wenyeji San Marino mabao 6-0 usiku huu Uwanja wa Olimpiki mjini Serravalle.
    Nahodha Wayne Rooney alianza kuifungia England kwa penalti dakika ya 13 na kuifikia rekodi ya mabao 49 ya Sir Bobby Charlton Three Lions.
    Beki wa San Marino, Cristian Brolli akajifunga katika harakati za kuokoa dakika ya 30 kuipatia England bao la pili, kabla ya Ross Barkley kufunga la tatu, akimalizia krosi ya Alex Oxlade-Chamberlain dakika ya 46.
    Theo Walcott akafunga la nne dakika ya 68 kabla ya Harry Kane kufunga la tano dakika ya 77. Walcott akashindilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la San Marino kwa bao la sita dakika ya 78.
    Kikosi cha San Marino kilikuwa; A. Simoncini, Bonini/Tosi dk72, Brolli, D. Simoncini/Aless. Della Valle dk80, Palazzi, Berardi; Hirsch, Battistini, Chiaruzzi, Vitaioli, Selva/Rinaldi dk75.
    England; Hart, Clyne, Stones, Jagielka, Shaw, Milner/Delph dk59, Shelvey, Barkley, Oxlade-Chamberlain/Walcott dk67, Rooney/Kane dk59 na Vardy.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ENGLAND YAFUZU EURO 2016, WALCOTT APIGA MBILI ‘SIMBA WATATU’ WAKIUA 6-0 SAN MARINO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top