MATOKEO MECHI ZA LIGI YA MABINGWA USIKU HUU
Chelsea 4-0 Maccabi Tel Aviv
Dinamo Zagreb 2-1 Arsenal
Roma 1-1 Barcelona
Olympiakos 0-3 FC Bayern Munchen
Valencia CF 2-3 Zenit St Petersburg
KAA Gent 1-1 Lyon
Dynamo Kyiv 2-2 FC Porto
Bayer 04 Leverkusen 4-1 BATE Borisov
Mshambuliaji wa Chelsea, Costa akishangilia na mchezaji mwenzake, Oscar baada ya kufunga bao la tatu PICHA ZAIDI GONGA HAPA
CHELSEA inayovurunda katika Ligi Kuu ya England, usiku huu imefufua makali na kuitandika mabao 4-0 Maccabi Tel Aviv ya Israel katika mchezo wa Kundi G Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Stamford Bridge, London.
Mabao ya The Blues inayofundishwa na Mreno Jose Mourinho yamefungwa na Willian Borges Da Silva dakika ya 15, Oscar dos Santos Emboaba Junior kwa penalti dakika ya 49, Diego Da Silva Costa dakika ya 58 na Cesc Fabregas dakika ya 78.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, Dynamo Kyiv imelazimishwa sare ya 2-2 na FC Porto Uwanja wa Olimpiki, Mabao ya Dynamo yamefungwa na Oleg Gusev dakika ya 20 na Vitaliy Buyalsky dakika ya 89 wakati ya Porto yamefungwa na Vincent Aboubakar dakika ya 23 na 81.
Nyota wa Barcelona, Lionel Messi akimpongeza Suarez baada ya kufunga bao la kuongoza PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Arsenal imechapwa mabao 2-1 na Dinamo Zagreb katika mchezo wa Kundi H, mabao ya wenyeji yakifungwa na Alex Oxlade-Chamberlain aliyejifunga dakika ya 24 na Junior Fernandes dakika ya 58, wakati The Gunners bao lao lilifungwa na Theo Walcott dakika ya 79 Uwanja wa Maksimir.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, Bayern Munich imeshinda 3-0 ugenini dhidi ya Olympiakos, mabao ya Thomas Muller dakika ya 52 na 90+2 kwa penalti, lingine likifungwa na Mario Gotze dakika ya 89 Uwanja wa Georgios Karaiskakis.
Kundi E; Bayer 04 Leverkusen imeshinda 4-1 dhidi ya BATE Borisov, mabao yake yakifungwa na Admir Mehmedi dakika ya nne, Hakan Calhanoglu dakika ya 47, Javier Hernandez ‘Chicharito’ dakika ya 58 na Hakan Calhanoglu kwa penalti dakika ya 75, wakati la BATE limefungwa na Nemanja Milunovic dakika ya 13 Uwanja wa BayArena.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, mabingwa watetezi, FC Barcelona wamelazimishwa sare ya 1-1 na AS Roma Uwanja wa Olimpico. Luis Suarez alianza kuifungia Barca dakika ya 21 kabla ya Alessandro Florenzi kuisawazishia Roma dakika ya 31.
Mshambuliaji wa Arsenal, Olivier Giroud akisikitika baada ya kutiolewa kwa kadi nyekundu timu yake ikilala 2-1 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Kundi H; Valencia CF imechapwa 3-2 na Zenit St Petersburg Uwanja wa Mestalla, mabao yake yakifungwa na Axel Witsel aliyejifunga dakika ya 54 na Andre Filipe Tavares Gomes dakika ya 73, huku mabao ya washindi yakifungwa na Givanildo Vieira de Souza dakika ya tisa na 44 na Witsel aliyesawazisha makosa yake dakika ya 76.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, KAA Gent imelazimishwa sare ya 1-1 na Lyon bao lao likifungwa na Danijel Milicevic dakika ya 68 baada ya Christophe Jallet kuanza kuifungia Lyon dakika ya 58 Uwanja wa Ghelamco.
0 comments:
Post a Comment