Nahodha wa Yanga SC, Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema anataka Ngoma awe mfungaji bora |
Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
NAHODHA wa Yanga SC, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema anakata mshambuliaji wao mpya, Mzimbabwe Donald Ngoma aongeze mabao na kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS-ONLINE jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Canavaro alisema hiyo ndiyo sababu alikataa kupiga penalti jana, Yanga SC ikishinda 3-0 dhidi ya Prisons Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wakiwa wanaongoza 2-0, Yanga wakapata penalti dakika ya 60 na kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm akamuita Cannavaro akapige, lakini beki huyo naye akaenda kumpa jukumu hilo Ngoma aliye katika msimu wake wa kwanza tangu asajiliwe kutoka FC Platinum ya kwao.
Na Ngoma akaenda kufunga bao lake la sita tangu atue Jangwani katika mechi ya 11 na kuifanya Yanga SC ishinde mechi ya pili mfululizo naye akifunga mechi ya pili mfululizo, baada ya awali pia kufunga katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Coastal Union Jumapili.
“Sijapingana na kocha, nilipenda Ngoma aipige ile penalti, ili aongeze mabao yake katika kuwania ufungaji bora. Na nilimuambia kocha akanikubalia,"amesema Cannavaro.
Mchezaji huyo kutoka visiwani Zanzibar alisema endapo Ngoma angekosa penati hiyo, basi angekubali kubeba lawama zote, kwani hakuchaguliwa na kocha Pluijm kufanya kazi hiyo.
Yanga SC inatarajiwa kushuka tena dimbani Jumamosi kumenyana na JKT Ruvu iliyofungwa mechi zote mbili za mwanzo Nyanda za Juu Kusini 1-0 na Majimaji na 3-0 na Mbeya City leo.
Baada ya hapo, wana Jangwani hao watakwenda kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu, Simba SC Septemba 26 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
NAHODHA wa Yanga SC, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema anakata mshambuliaji wao mpya, Mzimbabwe Donald Ngoma aongeze mabao na kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS-ONLINE jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Canavaro alisema hiyo ndiyo sababu alikataa kupiga penalti jana, Yanga SC ikishinda 3-0 dhidi ya Prisons Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wakiwa wanaongoza 2-0, Yanga wakapata penalti dakika ya 60 na kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm akamuita Cannavaro akapige, lakini beki huyo naye akaenda kumpa jukumu hilo Ngoma aliye katika msimu wake wa kwanza tangu asajiliwe kutoka FC Platinum ya kwao.
Na Ngoma akaenda kufunga bao lake la sita tangu atue Jangwani katika mechi ya 11 na kuifanya Yanga SC ishinde mechi ya pili mfululizo naye akifunga mechi ya pili mfululizo, baada ya awali pia kufunga katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Coastal Union Jumapili.
“Sijapingana na kocha, nilipenda Ngoma aipige ile penalti, ili aongeze mabao yake katika kuwania ufungaji bora. Na nilimuambia kocha akanikubalia,"amesema Cannavaro.
Mchezaji huyo kutoka visiwani Zanzibar alisema endapo Ngoma angekosa penati hiyo, basi angekubali kubeba lawama zote, kwani hakuchaguliwa na kocha Pluijm kufanya kazi hiyo.
Donald Ngoma (kushoto) alifunga kwa penalti jana Yanga SC ikishinda 3-0 dhidi ya Prisons |
Baada ya hapo, wana Jangwani hao watakwenda kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu, Simba SC Septemba 26 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment