// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BADO BAO MOJA TAMBWE KUANDIKA REKODI YA SIMBA NDANI YA YANGA SC - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BADO BAO MOJA TAMBWE KUANDIKA REKODI YA SIMBA NDANI YA YANGA SC - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, September 20, 2015

    BADO BAO MOJA TAMBWE KUANDIKA REKODI YA SIMBA NDANI YA YANGA SC

    REKODI YA AMISI JOSELYN TAMBWE TANZANIA
    Agosti 2013-Desemba 2014; Simba SC mechi26 mabao 43
    Desemba 2014 hadi sasa;  Yanga SC mechi 25 mabao 40
    (Jumla timu zote amecheza mechi 83 na kufunga mabao 51)
    Amissi Tambwe jana amefunga bao lake la 25 Yanga SC katika mechi ya 40 tangu atue Jangwani Desemba mwaka jana

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Burundi, Amissi Joselyn Tambwe amebakiza bao moja tu Yanga SC kufikisha idadi ya mabao yote aliyofunga alipokuwa Simba SC.
    Tambwe jana alifunga mabao mawili katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC ikishinda 4-1 dhidi ya JKT Ruvu na kufikisha jumla ya mabao 25 katika mechi 40 tangu atue Jangwani Desemba mwaka jana.
    Tambwe alicheza mechi 43 ndani ya msimu mmoja na nusu Simba SC na kufunga mabao 26 akiwa pia mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2013-2014, japokuwa Simba SC ilimaliza nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.
    Lakini jana Mrundi huyo amecheza mechi ya 40 tu Yanga na kufunga bao la 25- maana yake amekuwa na wakati mzuri zaidi Jangwani kuliko ilivyokuwa Msimbazi.
    Tambwe alifunga mabao 26 Simba SC katika mechi 43 ndani ya msimu mmoja na nusu

    Tambwe ni mchezaji ambaye hata mashabiki wa Simba SC walisikitika wakati anaachwa na kocha Mzambia Patrick Phiri ambaye alifukuzwa siku chache baadaye akaajiriwa Mserbia, Goran Kopunovic aliyeondoka pia mwishoni mwa msimu na kuajiriwa Muingereza Dylan Kerr.
    Tambwe alitua Simba SC Agosti mwaka 2013 pamoja na beki Mrundi mwenzake, Kaze Gilbert ambaye hata hivyo aliachwa baada ya nusu msimu. Na alitua Tanzania akitoka kuwa mfungaji bora wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame nchini Sudan sambamba na kuiwezesha Vital'O kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza. 
    Mkali huyo wa mabao, Tambwe atacheza mechi yake 41 Yanga SC itakapomenyana na mahasimu Simba SC Septemba 26 siku ambayo atawania kufikisha idadi ya mabao aliyofunga Msimbazi. 
    Tambwe akiwa na Kaze Gilbert wakipata chakula cha mchana na Mlimani City, Dar es Salaam baada ya kuwasili Agosti 20 kwa ajili ya kusaini Simba SC. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BADO BAO MOJA TAMBWE KUANDIKA REKODI YA SIMBA NDANI YA YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top