Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
HATIMAYE Azam FC imetangaza rasmi kuachana na winga wake wa kimataifa wa Uganda, Brian Majwega, na nafasi yake kuchukuliwa na Msenegal, Lacine Diouf.
Ofisa Habari wa mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati, Jaffar Idd Maganga ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE leo kwamba Majwega amerudishwa kwa mkopo katika klabu yake ya zamani ya KCC ya Uganda baada ya kukamilisha mazungumzo.
Idd amesema kwamba maamuzi hayo kumuondoa Majwega kikosini yalifanywa baada ya kufuata maelekezo kutoka katika benchi ya ufundi la mabingwa hao wa mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) ambalo liko chini ya Muingereza, Stewart Hall.
"Hivi tunavyozungumza hatuko naye mchezaji huyo na Azam ilifuata taratibu zote za kumtoa kwa mkopo katika timu yake ya zamani ya KCC," Idd alisema.
Sasa wachezaji wa kigeni wa Azam FC ni mabeki, Lacine Diouf, kiungo Jean Baptiste Mugiraneza wa Rwanda, beki Serge Wawa Pascal, kiungo Kipre Michael Balou, washambuliaji Kipre Herman Tchetche wote wa Ivory Coast, Didier Kavumbangu wa Burundi na Alan Wanga wa Kenya.
Kuhusu maandalizi kuelekea mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Jumamosi dhidi ya Prisons Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, Maganga amesema kikosi chao kinaendelea vizuri.
"Mazoezi yanaendelea vizuri, kwa bahati mbaya ni mchezaji mmoja tu, Michael Bolou, ndiye majeruhi na atakosekana katika mechi za awali za Ligi Kuu kuanzia Jumamosi,"amesema.
Winga wa kimataifa wa Uganda, alijiunga na Azam FC Desemba mwaka jana kutoka KCCA ya kwao na hadi anatolewa kwa mkopo, Majwega ameichezea timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa mechi 28 na kuifungia bao moja tu.

Brian Majwega (kulia) anatolewa kwa mkopo Azam FC baada ya kucheza mechi 28 na kufunga bao moja |

0 comments:
Post a Comment