MECHI ZA KESHO LIGI KUU TZ BARA
Yanga SC Vs Prisons
Mgambo JKT Vs Simba SC
Majimaji FC Vs Kagera Sugar
Mbeya City Vs JKT Ruvu
Stand United Vs Azam FC
Toto Africans Vs Mtibwa Sugar
Ndanda FC Vs Coastal Union
Alhamisi; Mwadui FC Vs African Sports
Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
AZAM FC imefunga safari kutoka Dar es Salaam hadi Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Kambarage, Shinyanga dhidi ya wenyeji, Stand United.
Kocha Mfaransa, Patrick Liewig amekalia kuti kavu baada ya kuanza vibaya Ligi Kuu kwa kipigo cha 1-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar Uwanja wa Kambarage Jumamosi.
Kocha huyo wa zamani wa Simba SC kesho atahitaji kurejesha amani ya kazi kwa kuhakikisha anashinda dhidi ya Azam FC iliyoanza kwa ushindi wa 2-1 nyumbani dhidi ya Prisons mjinj Dar es Salaam.
Hilo halitakuwa jepesi mbele ya kocha Muingereza wa Azam FC, Stewart Hall ambaye amepania kurejesha taji la ubingwa wa Ligi Kuu Chamazi.
Mabingwa watetezi, Yanga SC wataikaribisha Prisons ya Mbeya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kesho, wakati Mgambo JKT watakuwa wenyeji wa Simba SC Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Kagera Sugar walioanza kwa ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Mbeya City, watasogea kilomita kadhaa mbele Nyanda za Juu Kusini hadi Ruvuma kwenda kumenyana na Majimaji FC mjini Songea ambayo nayo ilianza na ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Ruvu.
Mechi nyingine za Ligi Kuu kesho ni kati ya Mbeya City na JKT Ruvu Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, Toto Africans na Mtibwa Sugar Uwanja CCM Kirumba mjini Mwanza na Ndanda FC dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Mechi za mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara zitakamilishwa keshokutwa kwa mchezo kati ya Mwadui FC dhidi ya African Sports Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Yanga SC Vs Prisons
Mgambo JKT Vs Simba SC
Majimaji FC Vs Kagera Sugar
Mbeya City Vs JKT Ruvu
Stand United Vs Azam FC
Toto Africans Vs Mtibwa Sugar
Ndanda FC Vs Coastal Union
Alhamisi; Mwadui FC Vs African Sports
Kikosi cha Azam FC kilichoifunga 2-1 Prisons katika mchezo wa kwanza Jumamosi Dar es Salaam |
Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
AZAM FC imefunga safari kutoka Dar es Salaam hadi Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Kambarage, Shinyanga dhidi ya wenyeji, Stand United.
Kocha Mfaransa, Patrick Liewig amekalia kuti kavu baada ya kuanza vibaya Ligi Kuu kwa kipigo cha 1-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar Uwanja wa Kambarage Jumamosi.
Kocha huyo wa zamani wa Simba SC kesho atahitaji kurejesha amani ya kazi kwa kuhakikisha anashinda dhidi ya Azam FC iliyoanza kwa ushindi wa 2-1 nyumbani dhidi ya Prisons mjinj Dar es Salaam.
Hilo halitakuwa jepesi mbele ya kocha Muingereza wa Azam FC, Stewart Hall ambaye amepania kurejesha taji la ubingwa wa Ligi Kuu Chamazi.
Mabingwa watetezi, Yanga SC wataikaribisha Prisons ya Mbeya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kesho, wakati Mgambo JKT watakuwa wenyeji wa Simba SC Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Kagera Sugar walioanza kwa ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Mbeya City, watasogea kilomita kadhaa mbele Nyanda za Juu Kusini hadi Ruvuma kwenda kumenyana na Majimaji FC mjini Songea ambayo nayo ilianza na ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Ruvu.
Mechi nyingine za Ligi Kuu kesho ni kati ya Mbeya City na JKT Ruvu Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, Toto Africans na Mtibwa Sugar Uwanja CCM Kirumba mjini Mwanza na Ndanda FC dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Mechi za mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara zitakamilishwa keshokutwa kwa mchezo kati ya Mwadui FC dhidi ya African Sports Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
0 comments:
Post a Comment