Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
KWA muda mrefu katika soko la usajili Tanzania ni Simba na Yanga SC ndiyo wamekuwa wakitawala kutokana na siyo tu kuwa zinapendwa sana, bali pia angalau zimekuwa zikitoa maslahi mazuri kulinganisha na klabu nyingine.
Mara chache kwa wakati tofauti zimetokea klabu za ‘kuzinyima usingizi’ Simba na Yanga katika soko la usajili, lakini ama hazikudumu au ziliamua kusalimu amri.
Wengi watakumbuka ile Malindi ya Zanzibar iliyokuwa chini ya ufadhili wa milionea Naushad Mohammed ilivyozipoteza Simba na Yanga SC katika soko la usajili.
Malindi ilichukua wachezaji tegemeo wa Yanga SC kiungo Nico Bambaga (sasa marehemu) na winga Edibily Lunyamila mwaka 1995 na kumzushia tafrani kubwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo ya Jangwani, George Mpondela ‘Castro’ (marehemu pia).
Hakuna uhakika kama imewahi kutokea timu nyingine ya ‘kuzitekenya korodani’ Simba na Yanga zaidi ya Malindi katika soko la usajili- kwa sababu Naushad alisifika kwa kutoa dau zuri la usajili.
Mlandege ya Zanzibar nayo chini ya ufadhili wa Abdul Sattar ilichukua wachezaji wa Simba SC, beki Alphonce Modest na kiungo Shaaban Ramadhani mwaka 1998, lakini wakati huo Wekundu wa Msimbazi wako ‘wamefulia’ na wanakabiliwa na migogoro.
Zimekuja baadaye Moro United ya milionea Merrey Balhaboub, lakini haikudumu na hiyo nayo haikuwahi kuziumiza sana kichwa Simba na Yanga katika soko la usajili.
Lakini sasa kuna timu ambayo inazilaza macho Simba na Yanga mara tu dirisha la usajili linapofunguliwa- hiyo si nyingine zaidi ya Azam FC ya bilionea Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake.
Azam FC ina uwezo wa kumchukua mchezaji yeyote imtakaye kutoka klabu yoyote Tanzania ikiamua na imekwishaonyesha mfano pale ilipomchukua kipenzi cha wana Yanga, Mrisho Ngassa mwaka 2009 kwa dau la rekodi dola za Kimarekani 50,000 wakati huo.
Dola 50,000 ambazo kwa sasa ni zaidi ya Sh. Milioni 100 walilipwa Yanga SC, hadi leo haijulikani Ngassa mwenyewe alilipwa kiasi gani, ila huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa maisha ya kifahari ya mchezaji huyo.
Wachezaji wengi hadi sasa wametoka Simba na Yanga SC kwenda Azam FC, lakini bahati moja mbaya ni kwamba ni Ngassa pekee ambaye unaweza kusema aling’ara Chamazi.
Jackson Chove, Obren Curkovick, Abdi Kassim ‘Babbi’ na Gaudence Mwaikimba ni wachezaji wengine walipita Yanga SC wakaenda Azam FC, lakini hawakuwahi kuwa muhimu kwenye klabu hiyo hadi walipoachwa.
Ramadhani Chombo ‘Redondo’, Jabir Aziz, Joseph Owino, Amri Kiemba, Uhuru Suleiman wote walitokea Simba SC kwenda Azam FC, lakini hawakung’ara hadi walipotemwa.
Didier Kavumbangu alikuwa ana msimu mzuri uliopita baada ya kusajiliwa kutoka Yanga SC, lakini dalili mbaya zimeanza mapema katika msimu wake huu wa pili.
Mrundi huyo amepoteza namba kikosi cha kwanza cha Azam FC mbele ya kocha Muingereza, Stewart Hall na anakabiliwa na changamoto kubwa mbele ya washindani wa nafasi yake, John Bocco, Kipre Tchetche, Ame Ali na Alan Wanga.
Mwishoni mwa dirisha la usajili zilivuma tetesi kwamba Kavumbangu angepelekwa kwa mkopo Simba SC, lakini diridha limefungwa na amebaki kikosini- swali je katika diridha dogo Desemba atapona?
Frank Raymond Domayo alisajiliwa kwa kishindo msimu uliopita kutoka Yanga SC kwa bahati mbaya kabla ya kuanza kucheza, ikagundulika ni majeruhi akaenda kufanyiwa upasuaji.
Amepona na ameanza kucheza tangu Februari, lakini hadi sasa bado hajaonyesha kuwa na amani- kwani hajawa na nafasi ya kudumu kikosini. Nini hatima yake naye? Tusubiri angalau hadi Desemba tutapata picha kama si kujua kabisa.
Azam FC imefunga dirisha la usajili msimu huu kwa kumsajili kwa kishindo pia winga wa Simba SC, Ramadhani Singano ‘Messi’ ambaye kwa bahati mbaya naye hajawa na mwanzo mzuri.
Kocha Stewart Hall hakumtumia kabisa katika kikosi kilichotwaa Kombe la Kagame mwezi uliopita Dar es Salaam na baada ya hapo katika michezo ya kirafiki amekuwa akitokea benchi zaidi.
Katika kutokea benchi, Messi amecheza mechi tano na kufunga bao moja- huku ikionekana kabisa anakabiliwa na ushindani mkubwa wa nafasi dhidi ya chipukizi akina Farid Mussa na wazoefu wenzake akina Khamis Mcha ‘Vialli’ na Kipre Tchetche.
Na hapo inakuwa nafuu kwake, Mganda Brian Majwega ameachwa- vinginevyo Messi angekuwa ana mlima mrefu sana wa kupanda kuwa mchezaji muhimu Azam FC.
Tumeona wachezaji wengi wa kutoka Simba na Yanga huwa hawawiki Azam FC, vipi Messi? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona.

Ramadhani Singano 'Messi' wakati anatambulishwa Azam FC Julai mwaka huu |

Mrisho Ngassa aliacha kumbukumbu nzuri Azam FC kabla ya kutolewa kwa mkopo Simba SC na baadaye kurejea Yanga SC. Kwa sasa anacheza Free State ya Afrika Kusini |
Wachezaji wengi hadi sasa wametoka Simba na Yanga SC kwenda Azam FC, lakini bahati moja mbaya ni kwamba ni Ngassa pekee ambaye unaweza kusema aling’ara Chamazi.
Jackson Chove, Obren Curkovick, Abdi Kassim ‘Babbi’ na Gaudence Mwaikimba ni wachezaji wengine walipita Yanga SC wakaenda Azam FC, lakini hawakuwahi kuwa muhimu kwenye klabu hiyo hadi walipoachwa.
Ramadhani Chombo ‘Redondo’, Jabir Aziz, Joseph Owino, Amri Kiemba, Uhuru Suleiman wote walitokea Simba SC kwenda Azam FC, lakini hawakung’ara hadi walipotemwa.
Didier Kavumbangu alikuwa ana msimu mzuri uliopita baada ya kusajiliwa kutoka Yanga SC, lakini dalili mbaya zimeanza mapema katika msimu wake huu wa pili.
Mrundi huyo amepoteza namba kikosi cha kwanza cha Azam FC mbele ya kocha Muingereza, Stewart Hall na anakabiliwa na changamoto kubwa mbele ya washindani wa nafasi yake, John Bocco, Kipre Tchetche, Ame Ali na Alan Wanga.
Mwishoni mwa dirisha la usajili zilivuma tetesi kwamba Kavumbangu angepelekwa kwa mkopo Simba SC, lakini diridha limefungwa na amebaki kikosini- swali je katika diridha dogo Desemba atapona?
Frank Raymond Domayo alisajiliwa kwa kishindo msimu uliopita kutoka Yanga SC kwa bahati mbaya kabla ya kuanza kucheza, ikagundulika ni majeruhi akaenda kufanyiwa upasuaji.
Didier Kavumbangu alifanya vizuri msimu wa kwanza, lakini msimu huu amekuwa akianzia benchi zaidi |
Mchezaji mpole na mwenye nidhamu, Amri Kiemba pia hakufanikiwa Azam FC |
Amepona na ameanza kucheza tangu Februari, lakini hadi sasa bado hajaonyesha kuwa na amani- kwani hajawa na nafasi ya kudumu kikosini. Nini hatima yake naye? Tusubiri angalau hadi Desemba tutapata picha kama si kujua kabisa.
Azam FC imefunga dirisha la usajili msimu huu kwa kumsajili kwa kishindo pia winga wa Simba SC, Ramadhani Singano ‘Messi’ ambaye kwa bahati mbaya naye hajawa na mwanzo mzuri.
Kocha Stewart Hall hakumtumia kabisa katika kikosi kilichotwaa Kombe la Kagame mwezi uliopita Dar es Salaam na baada ya hapo katika michezo ya kirafiki amekuwa akitokea benchi zaidi.
Katika kutokea benchi, Messi amecheza mechi tano na kufunga bao moja- huku ikionekana kabisa anakabiliwa na ushindani mkubwa wa nafasi dhidi ya chipukizi akina Farid Mussa na wazoefu wenzake akina Khamis Mcha ‘Vialli’ na Kipre Tchetche.
Na hapo inakuwa nafuu kwake, Mganda Brian Majwega ameachwa- vinginevyo Messi angekuwa ana mlima mrefu sana wa kupanda kuwa mchezaji muhimu Azam FC.
Tumeona wachezaji wengi wa kutoka Simba na Yanga huwa hawawiki Azam FC, vipi Messi? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona.
Athumani Iddi 'Chuji' aliwahi kufanya mazoezi na Azam FC, lakini hakusajiliwa |
0 comments:
Post a Comment