// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MABAO HABA LIGI KUU, KASEJA AANZA VIBAYA MBEYA CITY, ATUNGULIWA MOJA SOKOINE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MABAO HABA LIGI KUU, KASEJA AANZA VIBAYA MBEYA CITY, ATUNGULIWA MOJA SOKOINE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, September 12, 2015

    MABAO HABA LIGI KUU, KASEJA AANZA VIBAYA MBEYA CITY, ATUNGULIWA MOJA SOKOINE

    Azam FC imeshinda 2-1 dhidi ya Priosns leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam

    MATOKEO MECHI ZA UFUNGUZI LIGI KUU LEO

    Jumamosi Sept 12, 2015
    Simba SC 1-0 African Sports
    Ndanda FC 1-1 Mgambo Shooting
    Majimaji FC 1-0 JKT Ruvu 
    Azam FC 2-1 Prisons 
    Stand United 0-1 Mtibwa Sugar
    Toto Africans 1-0 Mwadui FC 
    Mbeya City 0-1 Kagera Sugar
    Kesho Septemba 13, 2015;
    Yanga SC Vs Coastal Union
    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    MABAO 10 tu yametinga nyavuni katika mechi  saba za ufunguzi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo, huku kipa mpya wa Mbeya City, Juma Kaseja akianza vibaya Uwanja wa Sokoine.
    Kaseja amefungwa bao moja  na timu yake mpya ikilala 1-0 nyumbani mbele ya Kagera Sugar kutoka Bukoba na hakuna timu iliyoshinda kwa wastani wa zaidi ya bao 1-0 dhidi ya wapinzani wake.
    Timu zote zote zimeshinda 1-0 na 2-1 baada ya mechi zote saba leo.
    Kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Simba SC imewafunga bao 1-0 wakati Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, Ndanda FC imelazimishwa sare ya 1-1 na Mgambo Shooting ya Tanga.
    Uwanja wa Majimaji, Songea  wenyeji Majimaji FC wameshinda 1-0 dhidi ya JKT Ruvu, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Azam FC imeshinda 2-1 dhidi ya Prisons wakati Toto Africans imeshinda 1-0 dhidi ya Mwadui FC.
    Timu zilizoanza kwa ‘mikosi’ zaidi Ligi ya msimu huu ni Stand United iliyofungwa 1-0 na Mtibwa Sugar Uwanja wa Kambarage, Shinyanga na Mbeya City iliyofungwa 1-0 na Kagera Sugar Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
    Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania itaendelea kesho wakati mabingwa watetezi, Yanga SC watakapomenyana na Coastal Union Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MABAO HABA LIGI KUU, KASEJA AANZA VIBAYA MBEYA CITY, ATUNGULIWA MOJA SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top