WIKI moja baada ya kutemwa timu ya taifa Togo, mshambuliaji Emmanuel Adebayor ametemwa pia na Tottenham Hotspur ya England rasmi leo na anakwenda kutuliza akili yake Ufaransa.
Kocha Mbelgiji wa Togo, Tom Saintfiet alisema hatamuita tena Adebayor kikosini mwake, baada ya kugomea wito wa mchezo wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika wiki iliyopita kufuatia kupokonywa Unahodha wa timu.
Aeebayor ambaye hajacheza mechi yoyote muhimu ya Spurs tangu January, bado hajaamua mustakabali wake na amepanda ndege kwenda Paris kwa mapumziko, ingawa zote West Ham United na Aston Villa zinamtaka mshambuliaji huyo ambaye amekuwa akifanya mazoezi na kikosi cha pili cha Tottenham.
Adebayor ameposti kwenye akaunti yake ya Twitter leo akisema amefikia makubaliano na uongozi wa klabu ya White Hart Lane kuvunja Mkataba baina yao ambao unamalizika mwishoni mwa msimu huu na sasa ni mchezaji huru.
Emmanuel Adebayor ameondoka Tottenham kama mchezaji huyu baada ya kufikia makubaliano ya kuvunja Mkataba
Adebayor ameposti katika akaunti yake ya Twitter akisema: "Naweza kuthibitisha kwamba nimefikia makubaliano na Tottenham Hotspur kuvunja Mkataba wangu.
"Napenda kuwashukuru klabu na mashabiki kwa muda wangu wote niliokuwa nao huko na nawatakia mema kwa msimu ujao,"amesema Adebayor ambaye aliambiwa mapema na kocha Pochettino kwamba hayumo kwenye mipango ya msimu huu ya Spurs.
Kocha wa Spurs, Mauricio Pochettino alimuambia Adebayor mapema kwamba hayumo kwenye mipango yake ya msimu huu
Adebayor, ambaye mambo yake yamekuwa Spurs chini ya kocha Mauricio Pochettino, amekuwa akitaka kulipwa Pauni Milioni 5 zote zilizobaki katika Mkataba wake ili aondoke.
Sasa mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester City na Arsenal forward atahitaji ruhusa maalum ya FIFA kujiunga na klabu nyingine, kwa kuwa alikwishapitishwa katika usajili wa Spurs kabla ya dirisha la usajili kufungwa mwezi huu.
0 comments:
Post a Comment