VIGOGO wa Misri, Zamalek wamemuongezea Mkataba kocha wao Mreno, Jesualdo Ferreira (pichani) kwa msimu mmoja zaidi.
Zamalek ilimchukua Ferreira Februari mwaka huu kwa Mkataba wa miezi sita baada ya kuondoka kwa Jamie Pacheco.
"Tumeanza majadiliano na Jesualdo Ferreira miezi miwili iliyopita kabla hajakubali Alhamisi kusaini Mkataba mpya wa mwaka mmoja,"amesema Mwenyekiti wa Zamalek, Mortada Mansour.
"Ni vizuri sana kwetu kubaki na kocha mzuri kama Ferreira kwenye timu. Tuna michuano ya Kombe la Misri na Kombe la Shirikisho (tunacheza). Tunapambana kushinda mataji hayo mawili na tuna na kocha huyo Mreno,".
Babu huyo wa umri wa miaka 69 ameiwezesha Zamalek kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Misri mwezi huu baada ya kuukosa kwa miaka 11.

0 comments:
Post a Comment