// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA SC YAWAPIGA BAO SIMBA SC, YAMSAJILI MKALI WA MABAO WA KMKM MATHEO SIMON - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA SC YAWAPIGA BAO SIMBA SC, YAMSAJILI MKALI WA MABAO WA KMKM MATHEO SIMON - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, August 09, 2015

    YANGA SC YAWAPIGA BAO SIMBA SC, YAMSAJILI MKALI WA MABAO WA KMKM MATHEO SIMON

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga SC wamemsajili mshambuliaji Matheo Anthony Simon kutoka KMKM ya Zanzibar.
    Habari ambazo BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE imezipata usiku huu ni kwamba mshambuliaji huyo hodari wa kufunga mabao amesaini Mkataba wa miaka miwili kuhamia Jangwani kikazi.
    Rasta huyo aliyefunga mabao mawili katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame wiki mbili zilizopita alikuwa anawaniwa pia na Simba SC.
    Matheo Anthony Simon (katikati) akisaini Mkataba wa Yanga SC leo. Kushoto ni Katibu wa Yanga SC, Dk. Jonas Tiboroha na kulia kiongozi wa KMKM



    Yanga SC iliamua rasmi kuisaka saini ya mchezaji huyo machachari japo hana umbo kubwa, baada ya kuifungia KMKM mabao mawili ikifungwa 3-2 na Simba visiwani Zanzibar katika mchezo wa kirafiki Jumatano. 
    Baada ya kusaini, Matheo kesho anasafiri kwenda Tukuyu, Mbeya ambako Yanga SC inayofundishwa na Mholanzi, Hans van der Pluijm imeweka kambi kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC Agosti 22.
    Matheo Anthony Simon kulia aling'ara kwenye Kombe la Kagame
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC YAWAPIGA BAO SIMBA SC, YAMSAJILI MKALI WA MABAO WA KMKM MATHEO SIMON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top