// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA SC YAMUUZA SHERMAN MILIONI 300, ASAINI MIAKA MITATU MPUMALANGA BLACK ACESS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA SC YAMUUZA SHERMAN MILIONI 300, ASAINI MIAKA MITATU MPUMALANGA BLACK ACESS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, August 03, 2015

    YANGA SC YAMUUZA SHERMAN MILIONI 300, ASAINI MIAKA MITATU MPUMALANGA BLACK ACESS

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI wa Yanga SC, Mliberia Kpah Sean Sherman amesaini Mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Mpumalanga Black Aces ‘AmaZayoni’ ya Afrika Kusini.
    Habari za ndani zinasema Yanga SC italipwa dola za Kimarekani 150,000 (Sh. Milioni 300) kama ada ya uhamisho ya mchezaji huyo aliyesaini Jangwani kwa dola 60,000 (Sh. Milioni 120,000) Desemba mwaka jana.
    Na Sherman aliyekuwa analipwa doka 3,000 (Sh. Milioni 6) kwa mwezi Yanga SC, sasa atakuwa analipwa dola 5,000 (Sh, Milioni 10) Black Aces kabla ya kukatwa kodi.
    Kpah Sean Sherman baada ya kusaini Black Acess juzi

    Mwenyekiti wa Aces, Mario Morfou ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE kwa simu leo kwamba wanatarajia Sherman atakuwa pacha mzuri wa Mzambia, Collins Mbesuma katika safu ya ushambuliaji ya timu yake msimu huu.
    “Ni mchezaji mzuri na mmoja wa wachezaji bora sana tuliowahi kusaini na sasa tunajivunia kuwa naye AmaZayoni,” amesema Morfou.
    Sherman alijiunga na Yanga SCS Desemba mwaka jana akitokea klabu ya Cetinkaya ya Ligi Kuu ya Cyprus Kaskazini na katika kipindi hicho ameichezea timu ya Jangwani mechi 27 na kuifungia mabao sita kwenye mashindano yote.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miak 23 sasa, alianza kuichezea Cetinkaya mwaka 2012, akitokea Duzkaya SK aliyoanza kuichezea mwaka 
    2010, akitokea Barrack YC ya nyumbani kwao, Liberia ambayo alianza kuichezea mwaka 2009.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC YAMUUZA SHERMAN MILIONI 300, ASAINI MIAKA MITATU MPUMALANGA BLACK ACESS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top