Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
YANGA SC imeachana na kiungo wake Hassan Dilunga, ambaye anahamia Stand United ya Shinyanga.
“Dilunga tumeachana naye moja kwa moja, tulitaka kumtoa kwa mkopo, yeye akataka tuvunjiane Mkataba bila masharti. Tumemkubalia na tumevunja Mkataba naye,”amesema Dk. Tiboroha.
Aidha, Tiboroha amesema kwamba beki Edward Charles amerudishwa JKT Ruvu kucheza kwa mkopo wa miezi sita hadi Desemba, wakati pia kuna uwezekano Hussein Javu akarudishwa Mtibwa kwa mkopo na beki Rajab Zahir akaenda kucheza kwa mkopo Stand United.
Wachezaji waliotemwa Yanga SC baada ya kumaliza mikataba yao ni Nizar Khalfan, Danny Mrwanda, Said Bahanuzi, Hamisi Thabit, Omega Seme na Jerry Tegete, wakati Mrisho Ngassa na Kpah Sherman wameondoka.
Ngassa amehamia Free State Stars na Sherman amehamia Mpumalanga Blac Aces, zote za Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
Wachezaji wapya waliosajiliwa Yanga ni; Mudathir Khamis, Benedicto Tinocco, Mwinyi Hajji Mngwali, Deus Kaseke, Matheo Anthony Simon, Godfrey Mwashiuya, Malimi Busungu, Vincent Bossou, Donald Ngoma na Thabani Kamusoko.
Tiboroha amesema kwamba kikosi cha Yanga SC kinaendelea na kambi yake Tukuyu mjini Mbeya na kinatarajiwa kurejea kesho jioni Dar es Salaam kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC mwishoni mwa wiki.
Kikosi cha Yanga SC kinaendelea na mazoezi mjini Mbeya na kinatarajiwa kurejea Dar es Salaam kesho jioni |
0 comments:
Post a Comment