MECHI ya Ngao ya Jamii kuashiria ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Azam FC na Yanga SC itachezwa Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salam na kiingilio cha chini kitakua ni Sh. 7,000.
Tovuti ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imetangaza viingilio vya mchezo huo, utakaoanza Saa 10:00 jioni, kuwa ni Sh 7, 000 kwa majukaa yenye rangi za kijani, bluu na chungwa, wakati VIP B na C itakuwa Sh. 20, 000 na VIP A Sh 30,000.
Tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa siku ya mchezo Jumamosi asubuhi Saa 2:00 katika maeneo ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

0 comments:
Post a Comment