KLABU ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya KOngo (DRC) imemsajili beki wa kati anayeweza kucheza kama kiungo pia, Badibake Mpongo.
Mchezaji huyo wa Sanga Balende amesaini Mkataba wa miaka mitatu kuhamia kwa mabingwa wa DRC, baada ya klabu yake kumalizana na Mazembe.
Na huyo anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na mabingwa wa Ligi Kuu ya DRC ambao kikosi wana Watanzania wawili, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.
Mazembe inaimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu ya DRC maarufu kama Linafoot na klabu imefurahia ujio wa mchezaji huyo ‘fundi’.
Kwa upande wake, Mpongo amesema; “Ni heshima kubwa kwangu kujiunga na TPM, klabu ambayo ni faraja ya nchi. Sasa naelekeza fikra zangu katika kucheza na kushinda mataji hapa,”amesema Badibake Mpongo, ambaye tayari ameanza mazoei na The Ravens.

Badiabake Mpongo kulia ametua TP Mazembe |
Mazembe inaimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu ya DRC maarufu kama Linafoot na klabu imefurahia ujio wa mchezaji huyo ‘fundi’.
Kwa upande wake, Mpongo amesema; “Ni heshima kubwa kwangu kujiunga na TPM, klabu ambayo ni faraja ya nchi. Sasa naelekeza fikra zangu katika kucheza na kushinda mataji hapa,”amesema Badibake Mpongo, ambaye tayari ameanza mazoei na The Ravens.
0 comments:
Post a Comment