// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TP MAZEMBE WAPAA KILELENI KUNDI A LIGI YA MABINGWA AFRIKA, USM ALGER YAWEKA REKODI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TP MAZEMBE WAPAA KILELENI KUNDI A LIGI YA MABINGWA AFRIKA, USM ALGER YAWEKA REKODI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, August 09, 2015

    TP MAZEMBE WAPAA KILELENI KUNDI A LIGI YA MABINGWA AFRIKA, USM ALGER YAWEKA REKODI

    Solomon Asante akishangilia baada ya kuifungia bao pekee TP Mazembe jana
    USHINDI wa bao 1-0 dhidi ya Smouha ya Misri jana mjini Lubumbashi umeipandisha kileleni mwa Kundi A timu ya Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
    Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Mazembe, bao pekee la TPM lilifungwa na Roger Assale dakika ya 53 na sasa mabingwa hao mara nne Afrika wanatimiza pointi nane baada ya kushinda mechi mbili na sare mbili.
    Washambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta alicheza mechi yote, wakati Thomas Emmanuel Ulimwengu alitokea benchi dakika ya 56 kuchukua nafasi ya Solomon Asante.
    Al Hilal ya Sudan inabaki na pointi zake tano baada ya juzi kufungwa 1-0 nyumbani na Moghreb Tetouan ya Morocco ambayo sasa nayo imefikisha pointi tano. Smouha ya Misri ina pointi tatu. 
    Mechi ya Kundi B iliyochezwa Ijumaa, USM Alger iliifunga 1-0 MC Eulma, zote za Algeria. 
    Hiyo ni mechi ya nne mfululizo UM Alger inashinda na sasa inafikisha pointi 12 kileleni, ikifuatiwa kwa mbali na El Merreikh ya Sudan yenye pointi nne.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TP MAZEMBE WAPAA KILELENI KUNDI A LIGI YA MABINGWA AFRIKA, USM ALGER YAWEKA REKODI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top