Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
TIMU ya Toto Africans ya Mwanza imeilaza bao 1-0 Kagera Sugar ya Bukoba jioni ya leo Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga katika michuano maalum ya timu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara za Kanda ya Ziwa.
Katika michuano huyo inayoandaliwa na Chama cha Soka Shinyanga (SHIREFA), kwa kushirikiana na kampuni ya Cleverland Res ya Mwanza, bao pekee la Toto lilifungwa na Waziri Junior dakika ya 80.
Mratibu wa mashindano hayo, Kabole Kahungwa ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE leo kwamba mechi hiyo ilikuwa kali na ya kusisimua na watu walifurahia burudani ya soka nzuri.
Katika mchezo wa ufunguzi jana, Mwadui FC iliwachapa ndugu zao, Stand United mabao 4-0 Uwanja huo huo wa Kambarage,
Mabao ya Mwadui yalifungwa na Zahoro Pazi dakika ya 50, Malika Ndeule dakika ya 58, Malegesi Mwangwa dakika ya 67 na Bakari Kigodeko dakika ya 80.
Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mchezo kati ya Mwadui na Toto, wakati keshokutwa Kagera itamenyana na Stand United.
RATIBA NA MATOKEO MICHUANO YA KANDA YA ZIWA
AGOSTI 9, 2015
Stand United 4-0 Mwadui FC
AGOSTI 10, 2015
Toto African 1-0 Kagera Sugar
AGOSTI 11, 2015
Mwadui FC Vs Toto Africans
AGOSTI 12, 2015
Kagera Sugar Vs Stand United
AGOSTI 13, 2015
Stand United Vs Toto African
AGOSTI 14, 2015
Mwadui FC Vs Kagera Sugar

Mfungaji wa bao pekee la Toto, Waziri Junior (kushoto) akiwa na Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Mjerumani Lucas Ftelimech baada ya mechi |
AGOSTI 9, 2015
Stand United 4-0 Mwadui FC
AGOSTI 10, 2015
Toto African 1-0 Kagera Sugar
AGOSTI 11, 2015
Mwadui FC Vs Toto Africans
AGOSTI 12, 2015
Kagera Sugar Vs Stand United
AGOSTI 13, 2015
Stand United Vs Toto African
AGOSTI 14, 2015
Mwadui FC Vs Kagera Sugar
0 comments:
Post a Comment