MABINGWA watetezi, Chelsea wameanza vibaya Ligi Kuu ya England baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Swansea City Uwanja wa Stamford Bridge, London usiku huu.
Oscar aliifungia bao la kwanza Chelsea kwa shuti la mpira wa adhabu ambalo lilipitiliza nyavuni dakika ya 23 kabla ya Andre Ayew, mtoto wa Mwanasoka Bora wa zamani Afrika, Abedi Pele kuisawazishia Swansea dakika ya 29.
Krosi ya Willian ilimbabatiza Federico Fernandez na kutinga nyavuni kuipatia Chelsea bao la pili dakika ya 30.
Kipa wa Chelsea, Thibaut Courtois alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 52 baada ya kumuangusha Bafetimbi Gomis kwenye boksi na mshambuliaji huyo Mfaransa akaenda kuisawazishia Swansea kwa penalti dakika ya 55.
Kikosi cha Chelsea kilikuwa; Courtois, Azpilicueta, Cahill, Terry, Ivanovic, Fabregas/Zouma dk76, Matic, Hazard, Oscar/Begovic dk54, Willian/Falcao dk84 na Costa.
Swansea City; Fabianski, Taylor, Williams, Fernandez, Naughton, Ki 5.5/Cork dk41, Shelvey, Sigurdsson, Montero/Routledge dk71, Ayew na Gomis/Eder dk79.
Thibaut Courtois akitoka nje baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kumuangusha Bafetimbi Gomis PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment