Ameposti kwenye Twitter picha hii |
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa England, Theo Walcott amesaini Mkataba mpya wa miaka minne kuendelea kuichezea Arsenal.
Katika Mkataba huo mpya, Walacott anaingia kwenye orodha ya wachezaji wanaolipwa zaidi kwenye klabu hiyo.
Mpachika mabao huyo wa England sasa atakuwa anaingiziwa kwenye akaunti yake benki Pauni 140,000 kila wiki sambambaa na nyota wengine wa The Gunners akina Alexis Sanchez na Mesut Ozil.
Walcott, ambaye ndiye mchezaji wa muda mrefu zaidi Arsenal alikuwa anasumbuliwa na majeruhi msimu uliopita, lakini kwa sasa yuko fiti na alifunga bao pekee la ushindi dhidi ya Wolfsburg wikiendi iliyopita katika Kombe la Emirates.
Theo Walcott amefurahia Mkataba wake mpya Arsenal kwa kuweka picha hizi zilizopigwa na mopiga picha wa klabu, Stuart MacFarlane PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment