// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TAIFA STARS YAANZA KUJIFUA BILA WA YANGA NA AZAM - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TAIFA STARS YAANZA KUJIFUA BILA WA YANGA NA AZAM - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, August 11, 2015

    TAIFA STARS YAANZA KUJIFUA BILA WA YANGA NA AZAM

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    KIKOSI cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kimeanza mazoezi katika uwanja wa Karume kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2017 nchini Gabon.
    Wachezaji wa Taifa Stars chini ya kocha wake mkuu Charles Mkwasa watakua wakijifua mara mbili kwa siku asubuhi na jioni katika uwanja wa Karume katika kujiweka fit na maandalizi ya mchezo huo.
    Kufuatia baadhi ya wachezaji kuwa na majukumu na timu zao kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Hisani utakaochezwa Agosti 22, Mkwasa amewaongeza wachezji wengine kumi (10) kutoka katika orodha yake ya akiba.
    Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa

    Lengo la kambi hii ya awali ya siku tano, ni kocha mkuu pamoja na benchi lake la ufundi kupata nafasi ya kuwaona wachezaji katika mazoezi hayo kabla ya safari ya kuelekea nchini Uturuki Agosti 23 mwaka huu kwa kambi ya siku kumi.
    Wachezaji walioitwa na kuanza mazoezi leo ni Said Mohamed, Vicent Andrew (Mtibwa Sugar), Mohamed Hussein, Ibrajim Hajibu (Simba SC), Hamis Ali, Juma Mbwana (KMKM), Tumba Sued (Coastal Unioni), Samuel Kamuntu (JKT Ruvu), Ibrahim Hilka (Zimamoto– Zanzibar) na Mohamed Yusuf (Prisons).
    Wachezaji wengine waliopo kambini ni Said Ndemla, Hassan Isihaka, Abdi Banda(Simba SC), Rashid Mandawa (Mwadui FC), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Orgeness Mollel (Aspire Academy) na Abdulhaman Mbambi (Mafunzo).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TAIFA STARS YAANZA KUJIFUA BILA WA YANGA NA AZAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top