// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TAIFA STARS YA BAADAYE KUJIPIMA LEO ZANZIBAR, TWIGA STARS NAO KUWEKA KAMBI HUKO HUKO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TAIFA STARS YA BAADAYE KUJIPIMA LEO ZANZIBAR, TWIGA STARS NAO KUWEKA KAMBI HUKO HUKO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, August 01, 2015

    TAIFA STARS YA BAADAYE KUJIPIMA LEO ZANZIBAR, TWIGA STARS NAO KUWEKA KAMBI HUKO HUKO

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    KIKOSI cha timu ya Taifa cha vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U-15) leo kinatarajiwa kushuka dimbani kisiwani Zanzibar kucheza michezo wa kirafiki na kombani ya kisiwani humo, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika mwaka 2017.
    Timu ya vijana ya Taifa wenye umri chini ya miaka 15 (U15) imekua ikiingia kambini kila mwisho wa mwezi kwa ajili ya kucheza michezo ya kirafiki ya kujipima nguvu, na kocha kupata nafasi ya kuona maendeleo ya vijana na kuongeza wachezaji wengine wanaonekana katika kuboresha kikosi hicho.

    Kikosi hicho cha Vijana cha U-15 kilichopo chini ya kocha mzawa Bakari Shime, kinajumuisha wachezaji 22 waliopo kambini, na kinatarajiwa kucheza michezo miwili kisiwani Zanzibari leo jumamosi na jumapili, kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam.
    Timu ya soka ya taifa ya Wanawake ya mpira wa miguu nchini Tanzania, Twiga Stars inatarajiwa kuingia kambini tarehe 04 Agosti kisiwani Zanzibar kwa gharama za TFF kujiandaa na Fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) zitakazofanyika nchini Congo Brazaville mwezi Septemba mwaka huu. 
    Aidha Kamati ya Utendaji imeiagiza sekretariet kuwasiliana na Kamati ya Olympic nchini (TOC) kuweza kujua mchango wao katika maandilizi hayo ya michezo ya Afrika.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TAIFA STARS YA BAADAYE KUJIPIMA LEO ZANZIBAR, TWIGA STARS NAO KUWEKA KAMBI HUKO HUKO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top