// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); STARS ITAREJESHA UZALENDO KWA USHINDI, SI KWA `MIDOMO YA MWEWE` - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE STARS ITAREJESHA UZALENDO KWA USHINDI, SI KWA `MIDOMO YA MWEWE` - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, August 05, 2015

    STARS ITAREJESHA UZALENDO KWA USHINDI, SI KWA `MIDOMO YA MWEWE`

    Na Hemed Kivuyo, DAR ES SALAAM
    WAPO baadhi ya watu (waandishi?)  wanaoropoka kwa kutumia vyombo wanavyofanyia kazi kwa muda kwa kuisifu Taifa Stars huku wakitoa maneno ya kuwafanya wanaowasikiliza kuamini kuwa ni Lazima waiunge Mkono Taifa Stars nani lazima waipende Taifa stars hata kama hawafanyi vizuri na tuache kuikosoa pale inapobidi.
    Wanataka tusiikosoe Taifa stars ama viongozi wake,wanataka tujigeuze `Kasuku` kuimba nyimbo wanazoimba wao ambazo hatujui wamepewa nini mpaka wakapata hiyo nguvu ya kuimba huo wimbo walazima.
    Wameacha kabisa kuelezea kiufundi Taifa stars inashindwa wapi na ifanye nini wanabaki kuimba `Uzalendo` kwani uzalendo ndiyo tatizo? Mbona huo ni ujuha!!

    Wao wamejibandika Nembo ya kuwazubaisha watu wsaiingalie stars kiufundi na badala yake wawaige wao kuimba Nyimbo za kipuuuzi.
    Timu yetu ya Taifa ( yasoka) haijaanza kushindwa leo,utakumbuka hata Rais Mstaafu al-hadji Ally Hassan Mwinyi aliwahi kukereka na kutamka neno `Kichwa cha mwenzawazimu`. 
    Hakukosea kutamka hilo neno ambalo sasa si tu ni `Kichwa cha Mwendawazimu` bali ni zaidi ya Kichwa cha Mwendawazimu.
    Stars inashindwa kwa mambo mengi sana,mojawapo ni Uongozi Mbovu ,ambao sasa wanatumia mbinu dhaifu kurejesha imani kwa watanzania jambo  ambalo nila `kitoto`.
    Viongozi  wanapaswa kuwa wabunifu na kuacha kuweka maslahi yao mbele na siyo kutafuta baadhi ya watu wenye akili fupi kama wao kutuimbisha wimbo wakipuuzi wakizalendo huku Timu yetu ya Taifa ikipoteza mwelekeo kila kukicha.
    Hivi karibuni Rais Jakaya KIkwete alipokuwa Bungeni Dodoma aligusia kuhusu kufubaa kwa Timu yetu ya Taifa ( Taifa stars) Rais wetu hakukosea kutamka aliyotamka  ambaye kila mwanamichezo alimsikia .
    Kwani ni uongo timu ya Taifa haikwenda mpaka Zanzibar lakini ikaendelea kufungwa? Si ilihama Dar es salaam!! Viongozi wa Soka kwa aibu yao walimwomba Rais wetu asihudhurie michezo ya timu ya Taifa eti akija huwa inafungwa!!! Wanatafuta mchawi nje ya uwanja!!! Huo ni umbilikimo wa fikra kama wanavyofanya sasa.
    Stars ni dhaifu kuanzia kwa viongozi wake mpaka baadhi ya wachezaji wake ,kama mzazi ni mlezi asiyejali familia unadhani mtoto atakuwa niwa namga gani baadaye? Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
    Taifa stars inaumwa masuala yakiufundi zaidi na namna yakuwafunda wachezaji wetu,stars yetu haiitaji watu wanaotulazimisha kurejesha uzalendo ili iifunge Nigeria,ili tuliamini hilo tusubiri muda utaongea.
    Makosa yanayofanywa na walinzi wa timu yetu na kusababisha tufungwe yanahitaji `kelele za uzalendo` ili makosa yasijirejee?? Ubutu wa ushambulizi wa Timu yetu inahitaji `kelele za uzalendo `ili safu iwe kali?  Kushindwa kwa viungo wetu kumiliki mpira muda mrefu na kugawa pasi za pembeni zinahitaji `kelele za uzalendo` ili wabadilike.
    Kukosa akili za soka kwa baadhi ya wachezaji wetu kunahitaji `kelele za uzalendo` kuwapa akili uwanjani?
    Timu kama Malawi au Nigeria wanaangalia makosa kwanza ili wayasahihishe na kuingia uwanjani,lakini sisi hatuangalii makosa badala yake tunatumia nguvu kubwa kuimba nyimbo zakijinga alafu tukifungwa tunatafuta wimbo mwingine!!
    Ni kwanini tusitumie Nguvu hizo kuwaimbisha umma kulaani mambo ya kidhalimu yanayofanywa na msanii `Shilole??? Acheni ujuha.
    (Mwandishi wa makala hii ni mtangazaji wa Redio One na ITV, anayepatikana kwa nambari +255 655 250 157 na +255 752 250 157)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STARS ITAREJESHA UZALENDO KWA USHINDI, SI KWA `MIDOMO YA MWEWE` Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top