Stewart Hall leo ameiongoza Azam FC kushinda mechi ya 10 mfululizo tangu arejee kwa mara ya tatu Juni mwaka huu
KOCHA Muingereza Stewart John Hall usiku huu ameiongoza Azam FC kushinda mechi ya 10 mfululizo tangu arejee kwa mara ya tatu Juni mwaka huu, baada ya kuifunga KMKM 1-0 Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Bao pekee la Azam FC katika mchezo wa leo limefungwa na beki Gardiel Michael Kamagi Mbaga kwa shuti la umbali wa mita 14 baada ya pasi ya Ramadhani Singano ‘Messi’.
Akiichezea kwa mara ya kwanza Azam FC tangu ahamie kutoka Simba SC mwezi uliopita, Messi alionyesha kiwango kizuri kuelekea mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga SC Agosti 22, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Azam FC imeweka kambi Zanzibar kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC wiki ijayo.
Wapinzani wao, Yanga SC wameweka kambi Tukuyu, Mbeya na leo pia walikuwa wana mchezo wa kirafiki, ambao wameshinda bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
0 comments:
Post a Comment