// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA SC, YANGA NA AZAM ZAONGEZEWA TENA MUDA WA KUSAJILI HADI MWISHO WA MWEZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA SC, YANGA NA AZAM ZAONGEZEWA TENA MUDA WA KUSAJILI HADI MWISHO WA MWEZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, August 11, 2015

    SIMBA SC, YANGA NA AZAM ZAONGEZEWA TENA MUDA WA KUSAJILI HADI MWISHO WA MWEZI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TAREHE ya mwisho ya kufunga dirisha la usajili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, imesogezwa tena mbele hadi Agosti 30 kwa ada ya Sh. 500,000 kwa kila mchezaji.
    Lakini klabu ambazo zitakamilisha usajili wa wachezaji wake Agosti 20, hazitalipwa fedha hizo.
    Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imesema kwamba baada ya awali kusogeza dirisha hilo kutoka Agosti 6, hadi 20, baada ya muda huo klabu itakayochelewesha kuleta usajili wake itatozwa kiasi cha shilingi laki tano (Tsh 500,000) kwa kila mchezaji itakayemsajili mpaka siku ya Agosti 30.
    Kocha wa Azam FC, Stewart Hall akiwa na kipa Muivory Coast, Vincent Angban ambaye kwa sasa yupo Simba SC kwa ajili ya kusajiliwa kufuatia 

    Mwisho wa kufanya uhamisho wa kimataifa wa wachezaji kwa njia ya mtandao TMS ni tarehe 6 Septemba.
    Kikao cha kamati ya sheria kitakaa tarehe 28 kwa ajili ya kuupitisha usajili na kitakaa tena tarehe 8/9/2015 kwa ajili ya kupitisha usajili.
    Kuanzia tarehe 21 hadi 27 itakuwa ni wiki ya pingamizi, ambapo majina yatabandikwa TFF Karume na kuwekwa kwenye mtandao ili kuwezesha vilabu vyenye pingamizi kuwawekea wachezaji mapingamizi.
    Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inatarajiwa kuanza tarehe 12 Septemba 2015, Daraja la kwanza (FDL) ikitarajiwa kuanza Septemba 17 na Ligi Daraja la pili inatarajiwa kuanza Oktoba 16 mwaka huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC, YANGA NA AZAM ZAONGEZEWA TENA MUDA WA KUSAJILI HADI MWISHO WA MWEZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top