RAIS wa Simba SC ya Dar es Salaam, Evans Elieza Aveva, mwishoni mwa wiki ametangaza uamuzi wa klabu yake kuachana na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo.
Aveva amesema Simba imefikia hatua hiyo baada ya klabu mbili za nchini Burundi kupandisha thamani ya mchezaji huyo na kuwa Sh. Milioni 200, badala 110 zilizokubakiwa awali.
Aveva alisema kwamba pamoja na jitihada za kutuma viongozi Bujumbura kwa mijadala mirefu, suala hilo limeshindikana na sasa wanaelekeza nguvu zao katika kusaka mchezaji mwingine.
Wakati Simba SC wakiugulia maumivu ya Mavugo, wapinzani wao katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC walikuwa wakifurahia kiwango kizuri kilichoonyeshwa na kinda Farid Malik Mussa katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Azam FC ilitwaa Kombe la Kagame mwishoni mwa wiki baada ya kuifunga mabao 2-0 Gor Mahia ya Kenya katika fainali na kinda Farid alikuwa ana mashindano mazuri ikiwemo kufunga bao pekee katika mchezo wa Nusu Fainali dhidi ya KCCA.
Farid alikuwa mmoja kati ya wachezaji wawili kwenye kikosi cha Azam FC ambao wamepandishwa kutoka katika akademi ya timu, mwingine Aishi Salum Manula.
Aishi ni kipa aliyedaka kwa ustadi mkubwa akimaliza mashindano bila kufungwa bao hata moja.
Leo hii kipa wa aina ya uwezo wa Aishi kwa hapa Tanzania mwingine nani? Tena kijana mdogo tu hadi kwa mwonekano, si kwa kuambiwa pekee.
Kwangu mimi, kwa sasa katika ukanda wetu huu wa Afrika Mashariki na Kati makipa bora ni wawili, Mganda Salim Magoola wa El Merreikh ya Sudan na Aishi.
Lakini pamoja na ukweli huo, Azam FC haikutoa mamilioni kwa wakati mmoja kumpata Aishi. Iliwekeza pole pole. Imemlea katika akademi kwa takriban miaka mitano, imemsomesha shule huku akiendelea kukuza kipaji chake na sasa inavuna matunda yake.
Vivyo hivyo kwa Farid, leo ukitaka winga wa uwezo wake utatajiwa ‘bei mbaya’, lakini Azam FC iliwekeza kidogo kidogo tu. Imemlea pale akademi, imemsomesha imeendeleza kipaji chake.
Na hao wa aina hiyo wapo wengi Azam FC, sote tunajua akina Bryson Raphael, Gardiel Michael Mbaga, Mudathir Yahya, Kevin Friday, Ismail Gambo ‘Kussi’ na Joseph Kimwaga wote tayari ni wachezaji wa timu kubwa ya Azam FC, lakini ni zao la akademi.
Na bado kuna wengine wanakuja huko chini, mfano kipa Metacha Boniphance Mnata ambaye alikuwemo kwenye orodha ya wachezaji 20 wa Kagame.
Azam FC sasa wanafurahia matunda ya kuwekeza katika soka ya vijana- na baada ya kumrejesha kocha Muingereza, Stewart John Hall ‘muumini’ wa vijana katika mpira wa miguu wanatarajia zaidi.
Azam FC sasa watanunua wachezaji kwa utashi tu, lakini zaidi wanatarajia kuwa Barcelona ya Tanzania. Na ndivyo tulivyoimaliza wiki iliyopita, Simba wanalia na Mavugo, Azam FC wanafurahia Farid. Siku njema.

0 comments:
Post a Comment