// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA SC INOGILE SIMBA DAY, SC VILLA ALALA 1-0 TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA SC INOGILE SIMBA DAY, SC VILLA ALALA 1-0 TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, August 08, 2015

    SIMBA SC INOGILE SIMBA DAY, SC VILLA ALALA 1-0 TAIFA

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    BAO pekee la Awadh Juma Issa dakika ya 89, limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya SC Villa ya Uganda katika mchezo wa kirafiki jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Katika mchezo huo wa kuhitimisha tamasha la Simba Day, Awadh alifunga bao hilo baada ya kuuwahi mpira uliorudi kufuatia kupanguliwa na kipa Stephen Odongo baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa SC Villa.
    Haukuwa ushindi mwepesi kwa Simba SC, kwani SC Villa walionekana kuwa wapinzani wagumu kwao tangu mwanzo, licha ya kucheza pungufu tangu dakika ya 44 baada ya Yoseri Waibi kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Ibrahim Hajib.
    Shujaa; Awadh Juma (kushoto) akikimbia kushangilia na Simon Sserunkuma


    Hamisi Kiiza 'Diego' wa Simba SC akipambana Mganea mwenzake, Henry Katongole wa SC Villa

    Simba SC ilianza kucheza soka ya kuvutia na kusisimua mashabiki wake kipindi cha pili, baada ya kocha Muingereza Dylan Kerr kufanya mabadiliko kadhaa.
    Waliobadili mchezo ni beki wa kushoto, Mrundi Emery Nimubona ambaye alikuwa anatia krosi maridadi zilizozua kizazaa langoni mwa wapinzani na Mwinyi Kazimoto ambaye alikwenda kuiongoza timu vizuri.
    Kipa Vincent Angban kutoka Ivory Coast alikuwa kivutio kutokana na kulinda vizuri lango la Simba, ikiwa ni pamoja na kuokoa michomo kadhaa ya hatari.
    Mshambuliaji Mganda Hamisi Kiiza ‘Diego’ aliyewahi kucheza kwa mahasimu, Yanga SC alikuwa mwiba kwa mabeki wa SC Villa, lakini alishindwa kufanya kitu kimoja tu- kutumbukiza mpira nyavuni.
    Pamoja na ushindi huo, kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kocha Kerr ana kazi nzito ya kufanya ili Simba SC ifikie katika ubora wa kuweza kushindania taji dhidi ya Azam na Yanga.
    Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Vincent Angban, Hassan Kessy/Emery Nimubona dk62, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’/Samih Hajji Nuhu dk75, Hassan Isihaka, Juuko Murushid, Justuce Majabvi, Said Ndemla, Ibrahim Hajib/Simon Sserunkuma dk46, Hamisi Kiiza/Danny Lyanga dk83, Mussa Mgosi/Boniphace Maganga dk84 na Peter Mwalyanzi/Mwinyi Kazimoto dk46.
    SC Villa; Stephen Odongo, Misi Katende,Yoseri Waibi, Henry Katongole, Paul Mbowa, Jonathan Mugabi, Godfrey Lwesibawa/Eturude Abel dk73, Martin Kiiza, Tokko Fahad/Kasumba Umaru dk66 na Robert Achema. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC INOGILE SIMBA DAY, SC VILLA ALALA 1-0 TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top