// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SHERMAN NA NGASSA USO KWA USO JUMAMOSI LIGI KUU AFRIKA KUSINI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SHERMAN NA NGASSA USO KWA USO JUMAMOSI LIGI KUU AFRIKA KUSINI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, August 04, 2015

    SHERMAN NA NGASSA USO KWA USO JUMAMOSI LIGI KUU AFRIKA KUSINI

    FREE State Stars yenye Mrisho Khalfa Ngassa na Black Aces yenye Kpah Sean Sherman zitakutana Jumamosi katika mchezo wa fungua dimba ya Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini.
    Free State ndiyo watakuwa wenyeji wa Blac Aces Uwanja wa Ground Goble Park mjini Bethlehem siku hiyo.
    Wawili hao, Sherman na Ngassa wote walikuwepo katika kikosi kilichotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Yanga SC msimu uliopita kabla ya kuhamia Afrika Kusini msimu huu. 
    Kwa mujibu wa ratiba ya msimu wa PSL wa 2015-16, mabingwa watetezi, Kaizer Chiefs wataanza kutetea taji lao dhidi ya Chippa United Agosti, Mamelodi Sundowns na Platinum Stars, Orlando Pirates na SuperSport United, wakati timu mbili zilizopanda msimu huu, Golden Arrows na Jomo Cosmos watakuwa nyumbani na University ya Pretoria na ugenini na Maritzburg United.
    Mechi ya pili, Ngassa kushoto atakutana na mabingwa wa ABSA, Kaizer Chiefs.
    Sherman baada ya kujiunga na Free State Stars 

    RATIBA YA MECHI ZA UFUNGUZI LIGI KUU AFRIKA KUSINI
    Free State Stars vs Black Aces
    Polokwane City vs Bloem Celtic
    Platinum Stars vs Mamelodi Sundowns
    Chippa United vs Kaizer Chiefs
    Bidvest Wits vs Ajax Cape Town
    Golden Arrows vs AmaTuks
    SuperSport vs Orlando Pirates
    Maritzburg United vs Jomo Cosmos
    Mrisho Ngassa baada ya kutua Free State Stars

    RAUNDI YA PILI LIGI KUU YA ABSA
    Raundi ya Pili ya Ligi Kuu ya Absa
    Orlando Pirates vs Chippa United
    Ajax Cape Town vs Maritzburg United
    AmaTuks vs Polokwane City
    Black Aces vs SuperSport United
    Kaizer Chiefs vs Free State Stars
    Mamelodi Sundowns vs Bidvest Wits
    Bloem Celtic vs Platinum Stars
    Jomo Cosmos vs Golden Arrows
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SHERMAN NA NGASSA USO KWA USO JUMAMOSI LIGI KUU AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top