Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KOCHA Muingereza, Dylan Kerr amemtema mshambuliaji Elias Maguri (pichani kushoto) baada ya kumjaribu katika mechi tatu akifunga mabao mawili- akidai kwamba mchezaji huyo anakosa sana mabao.
Kerr alimtumia Maguri katika mechi nne kwenye kambi ya visiwani Zanzibar wiki mbili zilizopita na mchezaji huyo akafunga mabao matatu, lakini haikumsaidia kumshawishi Muingereza huyo.
Kerr akawaambia viongozi wa Simba SC waachane na mchezaji huyo hamuhitaji katika kikosi chake.
Sababu? Kerr akawaambia viongozi wa Simba SC kwamba mchezaji huyo anapoteza nafasi nyingi za kufunga mabao.
Na akasema kwamba ana vijana wengi wa kikosi cha vijana, SImba B ambao anaweza kuwatayarisha kuwa washambuliaji wazuri kuliko Maguri.
Lakini uongozi ukamuambia, mchezaji huyo bado ana Mkataba wa mwaka mzima, hivyo akiachwa klabu italazimika kumlipa- na Kerr akawajibu; “Hata akibaki, hatacheza, atakuwa anafanya mazoezi tu,”.
Baada ya yote hayo, uongozi wa Simba SC ukakutana na Maguri na kumshauri atafute timu ya kucheza kwa mkopo kwa miezi sita ili kurudisha kiwango chake, labda anaweza kurejeshwa Msimbazi.
Simba SC bado wanasubiri jibu la Maguri kama atakwenda kwa mkopo sehemu nyingine, au ataamua vinginevyo.
Katika kipindi cha mwaka mmoja cha Maguri kuichezea Simba SC, amefunga mabao 12 katika mechi 43 za mashindano yote, zikiwemo za kirafiki.

Elias Maguri ameifungia Simba SC mabao 12 katika mechi 43 za mashindano yote |
Na akasema kwamba ana vijana wengi wa kikosi cha vijana, SImba B ambao anaweza kuwatayarisha kuwa washambuliaji wazuri kuliko Maguri.
Lakini uongozi ukamuambia, mchezaji huyo bado ana Mkataba wa mwaka mzima, hivyo akiachwa klabu italazimika kumlipa- na Kerr akawajibu; “Hata akibaki, hatacheza, atakuwa anafanya mazoezi tu,”.
Baada ya yote hayo, uongozi wa Simba SC ukakutana na Maguri na kumshauri atafute timu ya kucheza kwa mkopo kwa miezi sita ili kurudisha kiwango chake, labda anaweza kurejeshwa Msimbazi.
Simba SC bado wanasubiri jibu la Maguri kama atakwenda kwa mkopo sehemu nyingine, au ataamua vinginevyo.
Katika kipindi cha mwaka mmoja cha Maguri kuichezea Simba SC, amefunga mabao 12 katika mechi 43 za mashindano yote, zikiwemo za kirafiki.
0 comments:
Post a Comment