// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); PEDRO WA MAN UNITED ATOKEA BENCHI NA KUIPA BARCELONA 'NDOO KUBWA' YA UEFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE PEDRO WA MAN UNITED ATOKEA BENCHI NA KUIPA BARCELONA 'NDOO KUBWA' YA UEFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, August 12, 2015

    PEDRO WA MAN UNITED ATOKEA BENCHI NA KUIPA BARCELONA 'NDOO KUBWA' YA UEFA

    MCHEZAJI anayetakiwa na Manchester United, Pedro usiku huu ameifungia bao la ushindi Barcelona katika muda nyongeza na kuiwezesha kutwaa taji la Super Cup ya Ulaya.
    Katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Dinamo Arena mjini Tbilisi, Pedro alifunga bao hilo dakika ya 115 na kuifanya Barca ishinde 5-4 dhidi ya Sevilla, zote za Hispania.
    Ever Banega alianza kuwafungia mabingwa wa Europa League dakika ya tatu, kabla ya mipira miwili ya adhbu ya Lionel Messi dakika ya saba na 15 mabao ya Luis Suarez dakika ya 52 na Rafinha 44 kuifanya Barcelona iongoze 4-1.
    Jose Antonio Reyes akafunga dakika ya 57, Kevin Gameiro dakika ya 72 kwa penalti na Yevhen Konoplyanka dakika ya 81 kufanya dakika 90 zimalizike timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1.
    Lakini Pedro akatokea benchi dakika ya 93 kwenda kuchukua nafasi ya Mascherano na kuifungia bao la ushindi timu ya Luis Enrique dakika ya 81.
    Nyota anayetakiwa na Manchester United, Pedro akishangilia baada ya kuifungia Barcelona bao la ushindi katika mchezo wa Super Cup dhidi ya Sevilla usiku huu PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    Kikosi cha Barcelona kilikuwa; Ter Stegen, Dani Alves, Pique, Mascherano/Pedro 93, Mathieu, Rakitic, Busquets, Iniesta/Sergi Roberto dk63, Messi, Luis Suarez na Rafinha/Bartra dk78.
    Sevilla: Beto, Coke, Rami, Krychowiak, Tremoulinas, Krohn-Dehli, Banega, Reyes/Konoplyanka dk69, Iborra, Vitolo na Gameiro/Immobile dk80.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PEDRO WA MAN UNITED ATOKEA BENCHI NA KUIPA BARCELONA 'NDOO KUBWA' YA UEFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top