KOCHA Mkuu wa Nigeria, Sunday Oliseh amewaacha nyota wawili wa mabingwa wa England, Chelsea, John Obi Mikel na Victor Moses katika kikosi kitakachomenyana na Tanzania Septemba 5, mwaka huu kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika 2017.
Kiungo huyo wa zamani wa kimataifa wa Nigeria, amemuacha pia mshambuliaji wa Watford, Odion Jude Ighalo na Ogenyi Onazi.
Ighalo ameichezea dakika 106 katika mechi mbili za msimu huu wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Everton na West Bromwich Albion, lakini Mikel na Moses hawakuichezea Chelsea mechi mbili za mwanzo za msimu.
Hakuna sababu zilizotolewa juu ya kuachwa kwa wachezaji hao kwa ajili ya mechi na Tanzania, wakati pia mshambuliaji wa West Brom, Brown Ideye ni mchezaji mwingine mkubwa aliyetemwa kwa safari ya Dar es Salaam.
Oliseh ameamua kuita washambuliaji wengine sita, Ahmed Musa, Emem Eduok, Emmanuel Emenike, Anthony Ujah, Sylvester Igboun wa FC UFA ya Urusi na Moses Simon kuchukua nafasi za
Mikel, Joel Obi, Izunna Ernest Uzochukwu, Obiora Nwankwo, Lukman Haruna na Rabiu Ibrahim.
Kocha huyo mpya wa Super Eagles amemuita mshambuliaji wa Werder Bremen ya Ujerumani, Anthony Ujah kuja kuivaa Taifa Stars Septemba 5 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
Kikosi kamili cha Nigeria kitakachokuja Dar es Salaam kinaundwa na makipa; Vincent Enyeama (Lille OSC, Ufaransa); Carl Ikeme (Wolverhampton Wanderers, England), mabeki; Leon Balogun (FSV Mainz 05, Ujerumani); Kingsley Madu (AS Trencin, Slovakia); Godfrey Oboabona (Caykur Rizespor, Uturuki); William Troost Ekong (FK Haugesund, Norway) na Kenneth Omeruo (Kasimpasa SK, Uturuki)
Viungo ni; Joel Obi (Torino FC, Italia); Izunna Ernest Uzochukwu (FC Amkar Perm, Urusi); Obiora Nwankwo (Coimbra FC, Ureno); Lukman Haruna (Anzhi Makhachkala, Urusi); Rabiu Ibrahim (AS Trencin, Slovakia) na washambuliaji Ahmed Musa (CSKA Moscow, Urusi); Emem Eduok (Esperance ST, Tunisia); Emmanuel Emenike (Al Ain, UAE); Anthony Ujah (Werder Bremen, Ujerumani); Sylvester Igboun (FC UFA, Urusi) na Moses Simon (KAA Gent, Ubelgiji).

Victor Moses (kulia) na Obi Mikel kushoto wametemwa kikosi cha Nigeria kitakachoivaa mapema Tanzania mwezi ujao |

0 comments:
Post a Comment