// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NGASSA AANZA VIBAYA AFRIKA KUSINI, FREE STATE YACHAPWA 1-0 NYUMBANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NGASSA AANZA VIBAYA AFRIKA KUSINI, FREE STATE YACHAPWA 1-0 NYUMBANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, August 08, 2015

    NGASSA AANZA VIBAYA AFRIKA KUSINI, FREE STATE YACHAPWA 1-0 NYUMBANI

    Mrisho Ngassa (kulia) wakati anatambulishwa na kocha Kinnah Phiri FRee State baada ya kusajiliwa
    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa ameuanza vibaya msimu wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini, baada ya timu yake, Free State Stars kufungwa bao 1-0 na Mpumalanga Black Aces.
    Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Goble Park mjini Bethlehem, mshambuliaji mpya wa Blac Aces, Mliberia Kpah Sherman ambaye msimu uliopita alikuwa na Ngassa Yanga SC ya Dar es Salaam hakucheza.
    Bao pekee la wageni lilifungwa na Bhongolwethu Jayiya dakika ya 24 na kumpa mwanzo mzuri kocha Muhsin Ertugral klabu ya AmaZayoni mbele ya Ea Lla Koto.
    Stars waliowatumia Hendrick Somaeb mbele pamoja na wachezaji wapya Sthembiso Ngcobo na Mrisho Ngassa walitengeneza nafasi nzuri mwanzoni, wakashindwa kutumia.
    Kikosi cha Free State Stars kilikuwa: Diakite, Mashego, Sankara, Shabalala, Thlone, Somaeb, Masehe, Makhaula, Tshabangu/Mohomi dk55, Ngassa/Venter dk64 na Ngcobo/Masana dk72.
    Mpumalanga Black Aces: Mabokgwane, Kobola, Hendricks, Ngalo, Nonyane, Ngoma, Khuboni/Mashikinya dk88, Tukane/Mosemaedi dk67/Mtsweni dk90+3, Matsi, Jayiya na Mbesuma.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NGASSA AANZA VIBAYA AFRIKA KUSINI, FREE STATE YACHAPWA 1-0 NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top