// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MWASHIUYA APIGA MBILI, YANGA YAUA 4-1 KEMONDO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MWASHIUYA APIGA MBILI, YANGA YAUA 4-1 KEMONDO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, August 09, 2015

    MWASHIUYA APIGA MBILI, YANGA YAUA 4-1 KEMONDO

    Na Gwamaka Mwankota, MBOZI
    WINGA Godfrey Mwashiuya ametokea benchi na kuiadhibu timu yake ya zamani, Kemondo kwa kuifunga mabao mawili katika ushindi wa 4-1 jioni ya leo Uwanja wa CCM Mbozi, Mbeya.
    Yanga SC ilikwenda kupumzika ikiwa nyuma kwa bao 1-0, lakini kipindi cha pili kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm akabadilisha kikosi na timu ikapindua matokeo.
    Beki Juma Abdul alimpisha Mbuyu Twite, kiungo Thabani Kamusoko akampisha Said Juma ‘Makapu’, winga Deus Kaseke akampisha Mwashiuya na mshambuliaji Malimi Busungu akampisha Amisi Tambwe.
    Godfrey Mwashiuya (kulia) amefunga mabao mawili Yanga SC ikishinda 4-1 dhidi ya timu yake ya zamani Kemondo

    Mwashiuya aliyesajiliwa Yanga SC msimu huu kutoka Kemondo, akafunga mabao mawili, Simon Msuva na Tambwe moja Yanga ikishangilia ushindi wa 4-1.
    Yanga SC inaondoka Mbozi mara baada ya mchezo tu, kuelekea Tukuyu mkoani Mbeya pia, kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC Agosti 22, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
    Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Mudathir Khamis, Juma Abdul/Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Pato Ngonyani, Rajab Zahir, Thabani Kamusoko/Said Makapu, Simon Msuva, Salum Telela, Donald Ngoma, Malimi Busungu/Amisi Tambwe na Deus Kaseke/Godfrey Mwashiuya.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWASHIUYA APIGA MBILI, YANGA YAUA 4-1 KEMONDO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top